DC ATAKA TASISI ZIJIPANGE KUZALISHA KWA TIJA
MKUU wa wilaya ya mpwapwa
mkaoni Dodoma Bwana Jabil Shekimweli
namezitaka tasisi za serikali na tasisi
za umma wilayani hapa kuweza kutumia Agizo la kuhamia mjini Dodoma kama fursa ya kukuza uchumi wa tasisi zao kwa
kuongeza uzalishaji zaidi.
Sha kimweli aliyasema hayo
alipokuwa akiongea na wafanayakazi
wa tasisi ya ya utafiti wa mifugo TARILI Mpwapwa kwa lengo la kujitambulisha na kuzifahamu tasisi.
Mkuu wa wilaya huyo
alisema kuwa agizo la la serikali la kuhamia Mjini Dodoma lazima litafasiliwe kwa vitendo
na tasisi hizo kwa kuzalisha
kibiashara na kuongeza tija kwa
lengo la tasisi hizo kupata faida .
Aidha alisema kuwa
serikali ikiwa imeweka mkakati wa kuhami
mjini Dodoma lazima tasisi hiyo
ijiwekee mkakati wa
kuzalisha bidhaa zitokanazo na
mifugo kama maziwa,nyama kwa lengo
la kukuza uchumi wa Tasisi wa Wilaya
pia.
Aliongeza kuwa “unajua
ifikapo mwezi desember mwaka huu zaidi ya wafanyakazi wa serikali na tasisi za umma wapatao 100,000
watahamia Dodoma kutoka Dar –es-
salaam na hivyo wanahama na uchumi wao
usio pungua billion 1.2 hivyo ni kukua
kwa uchumi wa mji wa Dodoma ninyi kama tasisi lazima mjipange katika hizo
billion 1.2 mtachukua kiasi gani hapo
kwa kujiwekea mkakati mzuri wa uzaishaji”aliongea Shakimweli.
Pia alitaka tasisi kuweka
muunganiko na tasisi zingine
hapa wilayani ili kuweza
kuona matokeo ya tafiti zao
kwa wananchi wanao wanao izunguka
tasisi hiyo katika idara ya kilio na
mifugo.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa tasisi Dkt. Eliakunda Nkimbi alisema
ukosefu wa fedha unakwamisha shughuli za kitafiti kushidwa kufanyika na hivyo
kushidwa kutoa matokeo ya tafiti
kwa jamii.
Dkt. Nkimbi alisema endapo
serikali ikiwekeza katika tafiti za
wasomi changamoto nyingi zinazo ikabili
jamii zitapatiwa ufumbuzi wa changamoto zinazo wakabili kama ,umaskini wa
kipato, uhaba wa huduma za jamii, na uelewa
mdogo sera mbalimbali zinazotaka kuwapeleka katika unafuu wa maisha.
Comments
Post a Comment