SERIKALI INAOBWA KUWEKA SHERIA YA KULINDA HAKI ZA MAHOUSE GAIR.
SERIKALI imeobwa
kutunga sheria na kuzisimamia za kulinda
haki zawatumishi wa ndani ili kupunguza
vitendo vya unyanyasaji na
ukatili kwa watoto .
Rai hiyo ilitolewa ofisa ustawi wa
jamii wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa Bwana Richard Kiwale alipokuwa akiongea na Majira
ofisi kwake kwa mahojiano maluum.
Kiwale alisema siku
za hivi karibuni kumezuka vitendo vya
watoto kuuwawa na na wadada wasaidizi wa
ndani (house gair) kwa kile kinacho hisiwa kuwa ni hali ya kurudisha kisasi kwa
njisi wanavyo nyanyaswa na mabosi wao.
Aidha Kiwale alisema
kuwa Mabosi wengi wanao waaajili mabinti wa kuwasidia kazi za ndani wakuwa wakiwanyanyasa
na kuwatendea ukatili mabinti wao wa
ndani kitu alicho kisema kuwa kinachangia mabinti hao kurudisha kisasi kwa
watoto wanao walea kwa kuwachinja au
kuwachoma moto.
“watoto wengi ndio wamekuwa wakilea watoto wenzao na
hivyo baadhi ya mabos wamekuwa
wakiwanyanyasa sana wadada wa kazi kunyanyaswa sana kuwa kunyimwa haki zao
kama mshahara wa mwezi, chakula na
kutolewa maneno makali ambayo huwafanya watoto hao kukata tama na
kuwafanyia ukatili watoto wanao walea”aliongea
Kiwale.
Mmoja wa wazazi
wilaya hapa Bi Skai Thomas alisema kuwa ugumu wa maisha kunachangia sana kuongeza vitendo vya ukatili kwa watoto
kutokana na kuwatumia watu wa kati wa
kuwatafutia mabinti hao huko vijiji bila
kujua historia ya tabia yake .
Kwa upande wake mkuu
wa Dawati la njisia katika kituo cha
Polisi wilayani hapa Bi Elfrida Mapunda alikiri kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa
watoto hasa mabinti wa kazi za ndani kutokana na kuwa na umri mdogo na lakini bila kuwapo kwa sheria za kulinda
haki zao.
Pia aliongeza kwamba
lazima walezi na wazazi hapa nchini kujikita katika kusimamia haki za
mabinti wanao wasaidia kazi za ndani ili kuepuka vitendo mabyo vimeanza kusika kasi hivi karibuni vya watoto kuuwawa
na watoto wa mabosi wao.
Comments
Post a Comment