Na Stephen –noel –mpwapwa. WANANCHI wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameonyesha wasiwasi wao juu ya vitu vya kihistoria ya wilaya hiyo vilioachwa na wakoloni iko hatarini kutoweka kutokana na sehemu hizo za kihistoria kuto kuhifadhiwa na kulidwa na mamlaka husika. Wakiongea na waandishi wa habari mmoja wa wazee wakongwe wa mji huo bwana Abinoo Mathiasi mkazi wa hazina alisema kuwa miongoni mwa historia hizo ambazo ni njia kuu ya watumwa iliyokuwa ikotokea bara yaani mikoa ya Kigoma na Tabora na kuelekea Bagamoyo na Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Said Majid TippTip na Abushir ambayo kwa sasa iko mbioni kufutika Mti wa mlumbulumbu ambao kwa sasa umesha anguka na wanachi wameupasua kuni ambapo palichomwa kanisa la Anglikana la kwanza na mfanya biashara ya watumwa mwarabu Abushir kwa vile watu wa eneo hi...
BARAZA la madiwani katika halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa limeiomba ofisi ya ofisa madini mkazi Dodoma kuweza kuwajengea uwezo madiwani hao na wadau wanaofanya kazi za madini katika halmashauri hiyo ikiwa ni mkakati wa kukuza mapato ya ndani ya halmasahauri hiyo. Akisoma taarifa ya utekelezaji wa kamati ya fedha uongozi na mipango katika kipindi cha mwezi julai hadi septemba 2017 diwani wa kata ya Lumuma bwana Jocktan Cheliga amesema kuwa pamoja na wilaya ya Mpwapwa kuzungukwa na neema ya madini ya aina tofauti tofauti lakini wameshidwa kufaidika na rasilimali hiyo kutokana na madiwani wengi kuto kujua taratibu za upatikanaji wa mirahaba ya madini katika maeneo husika. Diwani wa kata ya Mazae bwana wiliamu Vahae akichangia mjadala katika kikao cha madiwani Mpwapwa. Mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana Donart Ngwezi amesema kuwa lazima kuwepo na ushirikiano wa pamoja kati...
Comments
Post a Comment