UHABA WA MAJI WASABABUISHA WATOTO WA NJE YA NDOA


MBUNGE wa jimbo la mpwapwa  George Lubeleje  ametoa siri ya chama cha
mapinduzi CCM kushidwa katika chaguzi ndogo katika kata ya Kingiti
kuwa ni uhaba wa maji safi na salama unao kikabili kijiji hicho.
LUbeleje amesema kuwa kijiji hicho kinakabiliwa na uhaba mkubwa wa
maji ambapo huwalazimu akina mama kuamka  usiku wa manane kwenda
kutafuta maji  kitu alicho kisema kuwa  kinapelekea wananchi wa kata
hiyo kukichukia chama cha mapinduzi na kupelekea kushidwa katika
chaguzi mbalimbali zinazo fanyika katika kata hiyo
Aidha Lubeleje  alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/ 2017
uongozi wa idara ya maji mjini hapa kuiweka kata hiyo  katika mpango
kata zitakazo kuwaaondolea akina mama kero ya kuamka usiku wa manane
kwenda kutafuta maji .
Alisema kutokana na hali ya uhaba wa maji katika kata hiyo kunapelekea
akina mama wengi kushidwa kufanya shughuli zingine za kimaendeleo na
kubaki katika  shughuli za kutafuta maji.
Kwa upande wake  Diwani wa kata Kingiti  Honarati Pima alisema  kuwa
akina mama wengi katika kata hiyo wamekuwa wakituhumiwa na waume wao
kuwa watoto  wanaowalea   sio wa kwao kwa kile alicho kisema
akina  mama wengi wanawapata watoto hao pindi wanapo kwenda kwenye
visima kutafuta maji.
“Akina mama wengi kwenye kata yangu wamekuwa wakilalamika kuwa wanalea
watoto ambao sio wao kutokana na akina mama wengi kumaka usiku wa
manane kwenda kutafuta  maji na kuwaaacha waume zao vitandani”alisema
diwani Pima.
Pima alisema kuwa  endapo kata hiyo ikipata maji itakuza  uchumi wa
kata hiyo  kwa kuweza kupata muda mrefu wa kufanya  shughuli zingine
za kuichumi kuliko kutumia muda mrefu kutafuta maji ya matumizi ya
nyumbani na wanyama.
Mwandisi wa maji  wa halamashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mwandisi Bahati
Haule alisema kuwa mwaka wa fedha 2016/2017 wilaya hiyo imepangiwa
shilingi bilion 1.4  lakini ambayo utekelezaji wake umekuwa mgumu
kuzipata hela hizo tangu waaambiwe wametengewa na wizara.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.