NDALICHAKO AJIONEA UCHAVU CHUO CHA UALIMU MPWAPWA.
CHUO cha ualimu Mpwapwa kinakabiliwa na uchakavu mkubwa ambao unatishia afya za watumishi na
wanafunzi chuoni hapo
Kufuatia uchakavu huo
waziri wa elimu ya sayansi , teknolojia na ufundi
Pr. Joyce Ndalichako aliutaka
uongozi wa chuo cha ualimu
Mpwapwa kuweza kufanya
tadhimini ya ukarabati mkubwa
wa chuo hicho kabla hakijanza kupokea
wanafunzi wa chuo kikuu cha
Dodoma.
Ndalichako aliyasema hayo
mwishoni mwa wiki aliotembelea
chuo hicho kujionea hali ya chuo hicho kabla chuo hicho hakiananza kupokea wanafunzi
walio kuwa wakisoma UDOM kuhamishiwa katika chuo
cha ualimu Mpwapwa kwa lengo la
serikali kukabiliana na chanagamoto ya ualimu wa sayansi hapa nchini.
Pr,Ndalichako
aliyasemna hayo mwishoni mwa
wiki alipotembelea chuoni hapo
kujionea hali ya chuo hicho ili
kukiweka tayari kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa mpango maluum wa walimu ya
masomo ya sayansi .
Pr.Ndalichako alisema
pamoja chuo hicho kuwa cha muda mrefu lakini kutokana na na tabia ya uongozi wa chuo hicho kuto
kufanya ukarabati wa mala kwa mala na kupelekea serikali kutumia pesa
nyingi kwa matengenezo .
Aidha Ndalichako
alisema baada ya ya chuo hicho kuteuliwa kupokea walimu wa masomo ya sayansi ambapo chuo hicho
kinakadiliwa kupokea wanafunzi 1100 wa masomo ya Sayansi ambao walikuwa wanafunzi wa chuo kikuu cha
Dodoma.
Kwa upande Mbunge wa
wa jimbo la Mpwapwa George Lubeleje amesema kuwa
chuo ni miongoni mwa
vyuo vikongwe hapa nchini
ambacho kilijegwa mwaka 1892
kikiwa na lengo la kuwaandaa
waafrika kukuza Elimu ya kilimo hapa nchini.
Hata hivyo kaimu mkuu wa chuo cha ualimu Mpwapwa Chacha Marwa
alisema kuwa kutokana na chuo hicho
kuwa cha Zamani hivyo kinakabiliwa na uchakavu
mkubwa anaotishia afya za wanafunzi na wafayakazi wake.
Pia mwalimu chacha alitanabaisha kuwa kuwa uchavu huo unahitaji zaidi ya shilingi
milini 500 li kuweza kukidhi hadhi ya
kuweza kutoa huduma bora ya masomo ya sayansi.
Mwalimu Chacha alisema
kuwa kwa sasa chuo hicho
kinakabiliwa na uchavu wa
miundombuinu yake kama viti,meza,vyumba vya madarasa, maabara, na nyumba za walimu.
Comments
Post a Comment