CHAMA chama cha walimu wilayani mpwapwa mkoani DODOMA kimepata viongozi wake wapya watakao kiongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano toka sasa. Viongozi hao waliopatikana kupitia kuchaguliwa na mkutano mkuu wa chama hicho, uliofanyika jana katika ukumbi wa chuo cha walimu mpwapwa mjini hapa . Akifungua mktano huo mkuu wa wilaya ya mpwapwa Dr Jasmini Tiisekwa alisema ni vyema walimu hao wakatumia haki yao ya kikatiba, kuwachagua viongozi wao ambao wataweza kushirikiana katika harakati za kumkomboa mwalimu na katika kuweza kujiletea maendeleo endelevu. Aidha Dr, Tiisekwa aliwaasa viongozi wa chama cha walimu hao kuweza kusimamia haki na wajibu wa wanachama wao ili kuweza kupunguza hali ya kutishia kwa kutoweka kwa amani hapa nchini kwa mada...