Posts

UMOJA WA WANAWAKE MPWAPWA WASAIDIA MADAWATI SHULE YA MSINGI VIGH'AWE .

Image
Kamati ya maandalizi ya Umoja wa  wanawake Wilaya ya Mpwapwa wakimuonyesha  Mgeni Rasmi moja ya dawati walilo tengeneza kwa ajili  ya  wanafunzi wa Shule  ya Msingi Vigh'awe waliokuwa wakisoma huku wakiwa wanakaa chini kwenye Sakafu.   Mgeni Rsmi Bwana Leo Mzeru  katika kwenye  sherehe ya maombi ya wanawake wa Kikiristo  Mpwapwa. Maandamo ya wanawake  katika viunga vya mji wa Mpwapwa kwenye sherehe za siku ya mwanamke Duniani, Na Stephen Noel- MPWAPWA  WANAWAKE WASAIDIA  WANAFUNZI WALIOKUWA WAKISOMA HUKU WAMEKAA CHIN I Wanawake wakikiristu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wameeaswa kuwa pamoja na kupambana na changamoto za kujikwamua kiuchumi laknini wasisashau majukumu yao ya kijinsia kama kulea na kunyonyesha watoto. Kauli hiyo imetolewa na mchungaji Nowadia zaidi kwenye mahubiri yake alipokuwa akiwahubiria akina wanawake kwenye sherehe za maombi ya umoja wa wananwake wa wakristu Mpwapwa iliyofanyika katika kanisa la watakatifu...

NESI AMBAKA MGONJWA AKIWA WODINI MPWAPWA.

Image
  JESHI la polisi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma limempandisha kizambani Bwana Athuman Kulwa (22) Kwa tuhuma za kumbaka Mgonjwa akiwa wodin. Mtuhumiwa huyo amefikishwa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nurupedesia Nassary akikabiliwa na kosa la kubaka . Akisomea shitaka lake mwendesha mashitaka wa polisi Bwana William Mwita aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyu alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 130kifungu kidogo (1) na cha (2)e na kifungu cha 131 kifungu kidogo (1) cha kanuni ya adhabu iliyofanyiwa malejeo mwaka 2919. Mwita aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kosa Hilo Juni 25 mwaka huu majira ya alfajiri katika wodi ya wogonjwa Katika hospitali ya wilaya ambapo alimbaka Eva Robert (40)Katika hospital ya Mpwapwa na mkoa wa Dodoma. Kwa upande wa mtuhumiwa aliikanusha shitaka lake na mwendesha mashitaka wa polisi aliiambia mahakama kuwa upepelezi wa kesi hiyo bado hivyo mahakaman ipange siku nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo namba 109 ya mwaka 2...

SERIKALI YAANZISHA BARAZA LA ARDHI MPWAPWA KUPUNGUZA MIGOGORO..

Image
KUTOKANA na kuwepo Kwa migogoro mingi ya Ardhi Katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Serikali inatarajia kuanzisha Baraza la Ardhi la wilaya ili kuweza kupunguza migogoro hiyo kwa Wakati. Aki zingumza na mwandishi wa habari ofisin kwake kwa mahojiano maluum afisa Ardhi na mali asili wa wilaya hii Anderson Mwamengo amesema kuwa wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya zinazo kabiliwa na migogoro mingi ya ardhi inayosababisha baadhi wa watu kuuwana .   Mwamengo amesema kufuatia hali  Serikali kupitia wizara husika inatarajia kuanzisha kwa Baraza la Ardhi kuanzia mwaka mpya wa Fedha "na tayari hatua za awali zimekamilika ikiwemo kuwateuwa wajumbe na mwenyekiti wa Baraza na miundo mbinu ikiwemo Baraza litakapo kuwepo. Alidai Kwa miaka mimwili mfululizo wamesajili zaid ya migogoro mia moja ya ardhi kutoka Katika maeneo tofauti ya wilaya "na migogoro hiyo mingi ilikuwa inasababishwa uelewa mdogo wa jamii juu umiliki pia baadhi ilikuwa inasababishwa na baadhi ya wajumbe wa ...

RAIS SAMIA ANAVYOPAMBANA NA MAADUI WA TAIFA UVCCM MPWAPWA.

Image
  Katibu w a vijana  wilaya ya Mpwapwa Isack Ngongi akiongea na vijana wa kata ya Ng'ambi  hawapo pichani.( Picha na Mpwapwa Habari ) SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO wa Tanzania chini ya Rais wake Samia Suluhu Hassan wameendelea kupambana na maadui watatu wa Taifa hili kwa kuboresha huduma za Jamii zikiwemo Elimu Afya na umaskin wa Kipato. Kauli hiyo hiyo imetolewa na Katibu wa jumuiya ya vijana wilayani Mpwapwa bwana Isack Ngongi alipofanya ziara ya siku moja katika Ng'ambi kuangalia. miradi ya Maendeleo na kuongea na vijana juu uundaji wa vikundi vya ujasilia mali, na ushiriki katika zoez la Sensa litakalo fanyika Agosti 23 mwaka huu. Ngongi amesema viongoz wote kuanzia mwalimu Nyerere wamekuwa wakipigana katika Kuboresha huduma za Jamii "lakini Rais wa awamu ya sita ndio kapiga bao la tiktaka kwa ujenzi wa vituo vya Afya  katika kata nyingi ambapo akina mama wajawazito wanajifungulia karibu, na kusababisha kupungua kwa vi...

TAKUKURU WAJA NA MBINU MPYA ZA MAPAMBANO YA RUSHWA.

Image
      Mpwapwa Uongozi wa Kata ya Mima na mkuu wa TAKUKURU WA pili kulia wakiwa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi  katika kata ya Mima. WANANCHI wa kata ya Mima mkoa wa Dodoma wameipongeza Tasisi   ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilayani Mpwapwa   kwa kuanzisha mpango   wa kuwafuata wananchi katika   maeneo yao   na kusikiliza kero zao zinaohusiana na masuala ya Rushwa na Utawala bora. Mmmoja wa wananchi   wa kata hiyo bwana Mathias Cosmas ametoa pongezi kwa uongozi wa TAKUKURU wilayani hapa  katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika kta ya Mima. Bwana Cosmas amesema mara nyingi   wananchi wanakuwa nakero zao   za kuhusiana na uongozi rushwa na utawala bora lakini wanashidwa kuzitoa kutokana na   umbali   au kuto kujua taratibu   za njisi ya kuwasilisha malalamiko hayo. Bwana Mathias amedai kuwa   hatua hiyo itasaidaia Tasisi kupata taarifa nyingi kwa wakati ...
Image
MPWAPWA Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Mpwapwa Bi Julieth Mtuy akiongea na madiwai hawapo pichani juu ya mada kuhusu Madhara ya Rushwa.  M KUU wa Tasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa wilaya Mpwapwa biJulieth Mtuy amewataka Madiwani wapya kuhakikisha   wanasimamia miradi ya Maendeleo kwenye Kata zao ili kuweza kuharakisha Maendeleo ya Mpwapwa. Bi Mtuy ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mada kwenye kikao cha Madiwani Jun ya athari za Rushwa katika Maendeleo ya mahari husika.  "Msimamie mapato yanayotokana na miradi iliyopo katika maeneo yenu, Kama vile miradi ya maji ili fedha zinazopatikana zilete tija na kuwainua wananchi kiuchumi"aliongea No Mtuy  Aidha amesema kuwa kwa sasa madiwani hao wameaminiwa na wananchi pamoja na chama hivyo wanawajibu wa kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia  sheria kanuni na maadili ya uongozi wao.  Pia amesema Ofisi yake haitavumilia  vitendo vyote vya  vinavyo ashiria Rushwa katika miradi na pesa za umma  a...

DC MPWAPWA AHIMIZA TEKNOLIJIA ITUMIKE KUPUNGUZA MALARIA NCHINI.

Image
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Mpwapwa.   Mkuu  wa wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, Mh. Jabir Shekimweri, amewaagiza wataalamu wa mifumo ya teknolojia hapa nchini kuang alia uwezekano wa kuitumia mifumo hiyo kwa kutoa elimu ya namna ya kudhibiti malaria hasa katika maeneo ya vijijini. Mh. Shekimweri ameyasema hayo wilayani Mpwapwa alikupowa akizindua mpango wa matumizi salama ya vyandarua vyenye dawa vilivyotolewa na Serikali kwa lengo la kutokomeza malaria hapa nchini mafunzo yaliyofanyika mjini Mpwapwa. Mkuu wa wilaya hiyo  amesema kwa nyakati  hizi, simu za mikononi zenye mitandao ya kijamii zimeenea kila mahala, hivyo ikiwepo namna nzuri ya kufikusha ujumbe utakaosaidia wananchi kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguuka, kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza mazalia ya mbu wanaosababisha maambukizi ya Malaria. Mafunzo hayo yamewashirikisha wataalamu mbalimbaalia kutoka wilaya za Kongwa na Mpwapwa ...