MPWAPWA
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Mpwapwa Bi Julieth Mtuy akiongea na madiwai hawapo pichani juu ya mada kuhusu Madhara ya Rushwa.
MKUU wa Tasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa wilaya Mpwapwa biJulieth Mtuy amewataka Madiwani wapya kuhakikisha wanasimamia miradi ya Maendeleo kwenye Kata zao ili kuweza kuharakisha Maendeleo ya Mpwapwa.
Bi Mtuy ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mada kwenye kikao cha Madiwani Jun ya athari za Rushwa katika Maendeleo ya mahari husika.
"Msimamie mapato yanayotokana na miradi iliyopo katika maeneo yenu, Kama vile miradi ya maji ili fedha zinazopatikana zilete tija na kuwainua wananchi kiuchumi"aliongea No Mtuy
Aidha amesema kuwa kwa sasa madiwani hao wameaminiwa na wananchi pamoja na chama hivyo wanawajibu wa kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia sheria kanuni na maadili ya uongozi wao.
Pia amesema Ofisi yake haitavumilia vitendo vyote vya vinavyo ashiria Rushwa katika miradi na pesa za umma alisema watazungukia kila kata kuongea na wananchi na kujua kero zao.
"TAKUKURU inaanzisha mpango wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi kwa kutembelea kata moja baada ya nyingine, na hivi karibuni tutaanza na kata ya Mima"
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakisikiliza MADA kuhusiana na masula ya Rushwa
Hata hivyo alisema alidai kuwa serikali ya awamu ya tano ikiwa inapambana na kuborsha na kitoa elimu bure kwa watanzania lakini baadhi ya madiwani na walimu wakuu"Rushwa isiwafanye kuwa viunganishi Kati ya wazazi wa mabinti waliopewa ujauzito na wazazi wa vijana wa kiume, Bali msimamie Sheria ichukue mkondo wake, na wahusika wapate adhabu inayostahili".
Mmoja wa wananchi wa wilaya ya Mpwapwa bwana Emanuel Ndule ame
sema Bado Rushwa imekuwa changamoto katika miradi mingi ya Maendeleo katika wilaya ya Mpwapwa ambayo inachangia Mpwapwa kuto kupiga hatua kimaendeleo.
sema Bado Rushwa imekuwa changamoto katika miradi mingi ya Maendeleo katika wilaya ya Mpwapwa ambayo inachangia Mpwapwa kuto kupiga hatua kimaendeleo.
"Kuna Mradi wa maji uliotoa maji siku tatu hadi Leo haijawahi kutoa kuna mradi wa ukumbi wa halmashauri umekwama kuna miradi mingi hapana tunawataka madiwani watimize kiapo chao na watekeleze ahadi walizo ziahidi kwa wananchi "aliongea Ema Ndule.
Pia Bi Tulakea Kimonga alisema kwa sasa sura mpya za madiwani wakiwamo vijana wengi wataisaidia Mpwapwa katika kuiletea Maendeleo.
Mwisho.
Comments
Post a Comment