RAIS SAMIA ANAVYOPAMBANA NA MAADUI WA TAIFA UVCCM MPWAPWA.
Katibu wa vijana wilaya ya Mpwapwa Isack Ngongi akiongea na vijana wa kata ya Ng'ambi hawapo pichani.( Picha na Mpwapwa Habari ) SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO wa Tanzania chini ya Rais wake Samia Suluhu Hassan wameendelea kupambana na maadui watatu wa Taifa hili kwa kuboresha huduma za Jamii zikiwemo Elimu Afya na umaskin wa Kipato. Kauli hiyo hiyo imetolewa na Katibu wa jumuiya ya vijana wilayani Mpwapwa bwana Isack Ngongi alipofanya ziara ya siku moja katika Ng'ambi kuangalia. miradi ya Maendeleo na kuongea na vijana juu uundaji wa vikundi vya ujasilia mali, na ushiriki katika zoez la Sensa litakalo fanyika Agosti 23 mwaka huu. Ngongi amesema viongoz wote kuanzia mwalimu Nyerere wamekuwa wakipigana katika Kuboresha huduma za Jamii "lakini Rais wa awamu ya sita ndio kapiga bao la tiktaka kwa ujenzi wa vituo vya Afya katika kata nyingi ambapo akina mama wajawazito wanajifungulia karibu, na kusababisha kupungua kwa vifo vya akina mama na watoto na kufikia maelengo ya milenium 2025 na mkakati wa Taifa wa kupunguza vifo vya akina mama na watoto. Aidha amedai ujenzi wa madarasa mengi kupitia fedha ya UVICO na kuondoa ada kuanzia kidato cha nne hadi cha sita ," lakini katika
kupambana na umaskini kuna mfuko wa Tasaf na mikopo isiyo na riba inayo
tolewa na halmashauri zote hapa nchini " alieleza. Amedai ili
kuweza kuchochoea Maendeleo endelevu vijana lazima wajitokeze mwenye zoezi la
Sensa linalokusudiwa kufanyika ogosti 23 mwaka huu. Baadhi ya vyumba vya madarasa vya shule ya Sekondari ya Ng'ambi vilivyo jengwa kwa fedha ya UVICO 19 . Milimo alisema pia
kwenye kata hiyo kuna miradi mingi inayoeendelea ikiwemo
miradi ya mabwawa ya maji na viwanda kwa ajili ya kukuza uchumi na Maendeleo
ya kata Ng'ambi.. Mwisho. |
Comments
Post a Comment