TAKUKURU WAJA NA MBINU MPYA ZA MAPAMBANO YA RUSHWA.
Mpwapwa
Uongozi wa Kata ya Mima na mkuu wa TAKUKURU WA pili kulia wakiwa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Mima.
WANANCHI wa
kata ya Mima mkoa wa Dodoma wameipongeza Tasisi
ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilayani Mpwapwa kwa kuanzisha mpango wa kuwafuata wananchi katika maeneo yao
na kusikiliza kero zao zinaohusiana na masuala ya Rushwa na Utawala
bora.
Mmmoja wa wananchi wa kata hiyo bwana Mathias Cosmas ametoa pongezi kwa uongozi wa TAKUKURU wilayani hapa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika kta ya Mima.
Bwana Cosmas
amesema mara nyingi wananchi wanakuwa
nakero zao za kuhusiana na uongozi
rushwa na utawala bora lakini wanashidwa kuzitoa kutokana na umbali
au kuto kujua taratibu za njisi
ya kuwasilisha malalamiko hayo.
Bwana Mathias
amedai kuwa hatua hiyo itasaidaia Tasisi
kupata taarifa nyingi kwa wakati na kuzitatua
papohapo kusaidia kuokoa pesa ya
serikali.
“Hata jina lenyewe
linasema kuzuia mngebaki huko mkisubiri kuwakamata mambo yanakuwa
wameharibika au mradi umeisha ndo
mnagundua mapungufu kwa sasa lazima
tulitambue tatizo mapema na kulishughulikia
kama wasemavyo kuwa lazima tushughulikie vyanzo vya tatizo na si
matokeo” ameongea
Aidha mmoja wa
wananchi katika kijiji hicho Bwana
Lameck Lenjima amedai kuwa kijiji
kero kubwa iko kwenye baraza la mogogoro la kata ambapo baadhi wa wajumbe wamekosa uaminifu na hivyo kushidwa kutoa maamuzi kwa haki na kutishia kutokea kwa vurugu kati
walegwa.
Pia ameiomba
tasisi ya hiyo kuweza kushughulikia
haraka chamnagomoto ya baadhi ya nyumba za kituo cha afya zilizo kuwa zimeungua ili wananchi waweze kujua muafaka wa pesa zao kutokana na Kituo hicho kinakabiliwa na
uhaba wa nyumba za wanganga na hivyo huwalazimu waganga kulala nje ya kituo na
kusabisha usumbufu kwa wagonjwa wa
dharula usiku.
Naye diwani
wa kata bwana Bezaleli Mnyabwa
amekili kuwapo kwa changamoto kubwa ya
malalamiko kutoka kwa baraza la migogoro ya kata kuto kufuata utaratibu na
kuwaonea baadhi ya watu hasa wanyonge kitu alichosema kinaweza kusabisha uvunjifu wa amani au mauwaji kwa wanao daiana
.
Naye Bi Jeny Maswala alidai wananchi wa kata hiyo huwalazima kutembea umbali wa zaidi ya
kilomita 30 kutafuta huduma za
kimahakama wakati kikogwe wa mika
88bwana Elia Chuga aliiomba wazee wa kijiji hicho kuingizwa kwe Mpango wa Tasaf
aili waweze kujikimu kimaisha.
Kwa upande wake
mkuu wa TAKUKURU Wilaya hiyo Bi Julieth
Mtuy amesema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa
wananchi kutoka vijijini hasa mengi ya malalamiko yanahusu migogoro ya
ardhi na maamuzi ya wajumbe kulalia
upande mmoja.
Hata hivyo Bi
Mtuy alisema wameamua kuwafuata wananchi vijini ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo,kuwaelimisha na kujikita
katika kuzuia sana kuliko kupambana zaidi.
“ Kwa sasa
tasisi itakuwa inazunguka katika kata kwa kutoa Elimu,lakini malalamiko mengi tunayoyapokea mengi yao utakuta
labda ni kuto kujua utaraibu tu hivyo tunakuja kuwajengea uwezo na kuwaelimisha lakini sio kwamba tumeacha
kukamata kwanza tunazuia na kupambana
ikiona tumefikia kwenye mapambano ujue kuwa tumekuelisha tumekufundisha
hukutusikiliza sasa ndo tunaingia kwenye
hatua ingine hivyo nawataka wanachi muendelee kutoa taarifa za ukweli na
viongozi kuweza kufuata taratibuna kanuni za kazi zenu” ameongea Bi Mtuy
Pia
amesema kwa kuhusu suala la kituo cha Afya Mima uongozi ngazi ya juu wanalifanyia
kazi na maamuzi yake yamefika hatua ambayo watapatiwa mrejesho siku si nyingi.
MWISHO.
Comments
Post a Comment