SERIKALI YAANZISHA BARAZA LA ARDHI MPWAPWA KUPUNGUZA MIGOGORO..




KUTOKANA na kuwepo Kwa migogoro mingi ya Ardhi Katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Serikali inatarajia kuanzisha Baraza la Ardhi la wilaya ili kuweza kupunguza migogoro hiyo kwa Wakati.

Akizingumza na mwandishi wa habari ofisin kwake kwa mahojiano maluum afisa Ardhi na mali asili wa wilaya hii Anderson Mwamengo amesema kuwa wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya zinazo kabiliwa na migogoro mingi ya ardhi inayosababisha baadhi wa watu kuuwana .  

Mwamengo amesema kufuatia hali  Serikali kupitia wizara husika inatarajia kuanzisha kwa Baraza la Ardhi kuanzia mwaka mpya wa Fedha "na tayari hatua za awali zimekamilika ikiwemo kuwateuwa wajumbe na mwenyekiti wa Baraza na miundo mbinu ikiwemo Baraza litakapo kuwepo.

Alidai Kwa miaka mimwili mfululizo wamesajili zaid ya migogoro mia moja ya ardhi kutoka Katika maeneo tofauti ya wilaya "na migogoro hiyo mingi ilikuwa inasababishwa uelewa mdogo wa jamii juu umiliki pia baadhi ilikuwa inasababishwa na baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya kata ya wilaya kushidwa kushauri vizuri na kuamua kwa kuzingatia maadili yao baadhi huendekeza upendeleo anaoweza kusababishwa na zawadi ndogo ndogo "alieleza.

Aidha Mwamengo amesema kabla ya kuanzishwa kwa Baraza hilo walakamikaji walikuwa wanalazimika kufuata haki katika wilaya ya Dodoma ambapo ilikuwa inawaghalimu pesa nyingi na muda na baadhi walikuwa wanashidwa kumudu ghalama  na kuacha haki zao kupotea na ilikuwa inaongeza migogoro na visasi kwa walakamikaji.


Afisa Ardhi na mali asili wa wilaya ya Mpwapwa Anderson Mwamengo

Mmoja wa wakazi wa wa wilaya hii   Bi Belitha Masasi amesema migogoro ya ardhi ilikuwa inachukua muda mrefu na baadhi ya Wananchi wengine walikuwa wanalazimika kuuza maeneo mengine ili kuweza kuendesha kesi hiyo.

Alisema  kuanzishwa kwa  Baraza hilo kutawasaidia Wananchi  wa wilaya ya Mpwapwa kupata haki zao za Ardhi kwa wakati na muda muafaka.

 

 



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.