DC MPWAPWA AHIMIZA TEKNOLIJIA ITUMIKE KUPUNGUZA MALARIA NCHINI.
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, Mh. Jabir Shekimweri, amewaagiza
wataalamu wa mifumo ya teknolojia hapa nchini kuangalia uwezekano wa
kuitumia mifumo hiyo kwa kutoa elimu ya namna ya kudhibiti malaria hasa
katika maeneo ya vijijini.
Mh. Shekimweri ameyasema hayo wilayani Mpwapwa alikupowa akizindua mpango wa matumizi salama ya vyandarua vyenye dawa vilivyotolewa na Serikali kwa lengo la kutokomeza malaria hapa nchini
mafunzo yaliyofanyika mjini Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya hiyo amesema kwa nyakati hizi, simu za mikononi zenye mitandao
ya kijamii zimeenea kila mahala, hivyo ikiwepo namna nzuri ya kufikusha
ujumbe utakaosaidia wananchi kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguuka,
kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza mazalia ya mbu wanaosababisha maambukizi
ya Malaria.
Mafunzo hayo yamewashirikisha wataalamu mbalimbaalia kutoka wilaya za
Kongwa na Mpwapwa mkoani Dodoma wakiwemo Wakuu wa Vituo vya Polisi kutoka
katika wilaya hizo mbili.
Comments
Post a Comment