NESI AMBAKA MGONJWA AKIWA WODINI MPWAPWA.
JESHI la polisi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma limempandisha kizambani Bwana Athuman Kulwa (22) Kwa tuhuma za kumbaka Mgonjwa akiwa wodin. Mtuhumiwa huyo amefikishwa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nurupedesia Nassary akikabiliwa na kosa la kubaka . Akisomea shitaka lake mwendesha mashitaka wa polisi Bwana William Mwita aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyu alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 130kifungu kidogo (1) na cha (2)e na kifungu cha 131 kifungu kidogo (1) cha kanuni ya adhabu iliyofanyiwa malejeo mwaka 2919. Mwita aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kosa Hilo Juni 25 mwaka huu majira ya alfajiri katika wodi ya wogonjwa Katika hospitali ya wilaya ambapo alimbaka Eva Robert (40)Katika hospital ya Mpwapwa na mkoa wa Dodoma. Kwa upande wa mtuhumiwa aliikanusha shitaka lake na mwendesha mashitaka wa polisi aliiambia mahakama kuwa upepelezi wa kesi hiyo bado hivyo mahakaman ipange siku nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo namba 109 ya mwaka 2022 inayomkabili mtuhumiwa huyo inasikilizwa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mpwapwa Nurupedesia Nassary. Aidha Mhe Nassary aliniambia mahakama kuwa dhamana ya mtuhumiwa iko wazi kama atatimiza masharti ya dhamana Kwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya nida na watasaini dhamana yenye samani ya shilingi milioni tatu kila mmoja. Mtuhumiwa alitimiza masharti ya dhamana na kachiliwa kwa kutimiza masharti ya dhamana hadi hapo tarehe 25 mwezi wa 7 kesi yake itakapo tajwa tena. Mwisho. |
Comments
Post a Comment