UMOJA WA WANAWAKE MPWAPWA WASAIDIA MADAWATI SHULE YA MSINGI VIGH'AWE .

Kamati ya maandalizi ya Umoja wa  wanawake Wilaya ya Mpwapwa wakimuonyesha  Mgeni Rasmi moja ya dawati walilo tengeneza kwa ajili  ya  wanafunzi wa Shule  ya Msingi Vigh'awe waliokuwa wakisoma huku wakiwa wanakaa chini kwenye Sakafu.




 Mgeni Rsmi Bwana Leo Mzeru  katika kwenye  sherehe ya maombi ya wanawake wa Kikiristo  Mpwapwa.



Maandamo ya wanawake  katika viunga vya mji wa Mpwapwa kwenye sherehe za siku ya mwanamke Duniani,

Na Stephen Noel- MPWAPWA 

WANAWAKE WASAIDIA  WANAFUNZI WALIOKUWA WAKISOMA HUKU WAMEKAA CHINI

Wanawake wakikiristu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wameeaswa kuwa pamoja na kupambana na changamoto za kujikwamua kiuchumi laknini wasisashau majukumu yao ya kijinsia kama kulea na kunyonyesha watoto. Kauli hiyo imetolewa na mchungaji Nowadia zaidi kwenye mahubiri yake alipokuwa akiwahubiria akina wanawake kwenye sherehe za maombi ya umoja wa wananwake wa wakristu Mpwapwa iliyofanyika katika kanisa la watakatifu wote Anglikana Vigahwe.

 Amesema pamoja na kupambana na chanagamoto za Ukatili wa Kijinsia ,mfumo dume, na mila kandamizi bali wasisasahau majukumu yao kama maandiko yanavyo wataka ambapo alisema baadhi ya akina mama wanaogopa kuwanyonyesha watoto kwa madai ya kwamba wataharibu maumbile ya kama maziwa kuanguka. Amedai kwamba Mungu aligawa majukumu ya mwanaume na mwanamke kwa sababu za msingi na makasudi makubwa ‘’ Mungu aliweza kumpa kila mwanadamu majukumu yake kwa lengo na makusudi maluum hivyo kila mmoja atimize wajibu wake katika familia na ndoa ili dunia iwe mahali salama pa kuishi.


Baadhi ya madawati yaliyo nunuliwa na umoja wa wanawake wa Kikristu  kwa ajili ya  wanafunzi wa shule ya msingi Vigh'awe.


 Mwenyekiti wa umoja wa wananwake wakrito Mpwapwa Mwl. Grace Mpoyola amedai kwamba kwa mwaka huu umoja wa wananwake Mpwapwa umesaidia kuchangia madawati kumi katika shule ya Msingi vig’hawe ambayo hukabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati huku watoto wakiwa wanasoma huku wanankaa chini kwenye sakafu. Amesema pia kwa mwaka huu wameliombea Taifa katika harakati za kupanda kwa bei za vitu hasa vyakula vinavyopelekea baadhi ya familia kuwakimbia watoto na kuwaaacha wenyewe wakijilea.


 Aliyekuwa mgeni Rasmi katika hafala hiyo Bwana Leo Mzeru aliwataka wanawake kuweza kutimiza majukumu yao kwa kadri ya maadiko na Imani wanazo ziamini hasa jukumu la kuwalea watoto ili kuweza kupata taifa lenye maadili na hofu ya Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.