Posts

DC MPWAPWA AMESEMA HAKUNA MTU ATAKAYE KUFA KWA COVID 19KAMA WATAZINGATIA MAELEKEZO YA WATAALAM.

Image
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri  Akiongea na Mwandishi wa habari hizi ofisi kwake. Picha na Mpwapwa Habari. Na Stephen Noel . Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bwana Jabiri Shekimweri amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA CIVID- 19   na wasitishwe na mamneno ya mitandao juu ya ugonjwa huo. Mkuu wa wilaya ameyasema hayo jana ofisi kwake akifanya mahojiani na   na mwandishi wetu juu ya mkakati wa wilaya thidi ya kujikinga na    maambukizi ya ugonjwa   huo ambao   kwa sasa umekuwa ni janga la kimataifa. Shekimweri amesema   lazima   wananchi   waelewe na kuendelea kuchukua tahadhari thidi ya ugonjwa huo   ambapo kama “ kama wilaya tayari tumesha fanya uhamasishaji katika makundi yote yanayo tuzunguka   wakiwemo wafanya biasahara bodaboda   masokoni makanisani na misikiti juu ya kujenga uelewa kwa jamii na njia za kujinga ...

Madiwani wa wakumbushwa kujaza tamko la mali pindi udiwani unapokoma.

Image
Mpwapwa.   Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri yua Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, wamekumbushwa kujaza za maadili na kuwasilisha Matamko   ya Mali yao na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma pindi Udiwani wao unapokoma mwezi Julai 2020. Hayo yalisemwa na Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. George Shilla wakati akiwasilisha mada ya Tamko la Mali na Madeni katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halimashauri ya Wilaya ya Mpwapwa juzi. “Jukumu la kujaza   fomu ya maadili   ni jukumu la kila kiongozi wa umma   na halimuhusu mwajiri wake au mkuu wake wa idara hivyo kujaza fomu hizi ni takwa la   kisheria     ya Maadili namba 13 ya Mwaka 1995 inayomtambua Kiongozi wa Umma binafsi kila mmoja na sio hiyari ya kiongozi” alifafanua bwana Shilla. Aidha Bw. Shilla alidai kuwa     Madiwani wana wajibu wao wa kuwasilisha fomu hizo kwa Kamishna wa Maadili   wenyewe na siyo...

WAZIRI WA MAMNBO YA NDANI YA NCHI ATANGAZA NEEMA KWA BODABODA.

Image
MPWAPWA. WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi Mhe George Simbachawene   amepiga marufuku kwa polisi kukamata wananchi,bodaboda       na kuwanyanyasa   na pia amepiga marufuku   kufanya oparesheni yoyote ndani ya mkoa au wilaya   bila kuwashirikisha wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama. Simbachawene ametoa kauli hiyo wilayani Mpwapwa alipokuwa kwenye ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza na madiwani wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa. Simbachawene amesema kuna baadhi ya polisi wamekuwa wakikiuka   taratibu   na kanuni za kipolisi kwa kuwakamata wananchi na hasa madreva wa pikipiki   maarufu kama bodaboda   kwa kisingizio kama mimi nimewatuma “ kuanzia leo kupitia hapa Mpwapwa natangaza bodaboda wasisumbuliwe na   kukamatwakamatwa pasipo kuwa na sababu za msingi” alizungumza . Pia amewataka bodaboda wote nchi kuweza   kuzingatia sheria za usalama barabarani   ili kuweza kupunguza ajari na kuwe...
Image
MPWAPWA -MICHEZO Walimu wa michezo Nchini wametakiwa  kutoa fursa sawa kwa vijana wenye viapaji  wa mjini na vijijini ili kuweza kufikia ndoto zao kimchezo kama walizofikia wachezaji wakubwa wa kimataifa. Kauli hiyo ilitolewa na ofisa Elimu Sekondari  wilaya  ya Mpwapwa bwana Nelson Milanzi  katika zoezi la kufunga kozi ya siku tatu kwa walimu wa wa michezo wa wilaya ya Mpwapwa. Mwalimu Milanzi  alisema michezo ikiwekwezwa vizuri kwa watoto  vijana inaweza ikapunguza changamoto  ya ajira kwa  kwa vijana  katika taifa letu “hasa kwa wale wenye vipaji  hasa wale walioko pembezoni kwa mfano akina Mbwana Samata  waliotokea mbagala huko mbona hutuwasikii vijana wenye vipaji wanaotoka vijijini  inaamana hawako wenye vipaji huko sasa nyie nendeni mkawatengeneze akina Samata wengi ” Naye  mkufunzi wa kozi hiyo Bwana Charles Maguzu  aliwataka Walimu wa michezo  katika shule   ...
Image
Mwl.Augusta Lupokela kaimu mkurugenzi msaidizi wa mafunzo ya ualimu ,Wizara ya Elimu Sayansi na Tecknolojia. MBUNGE wa Jimbo la Mpwapwa   Mhe George Lubeleje (Seniour MP) ameiomba serikali kuweza   kutenga Bajeti ya kutosha    katika sekta ya michezo   nchini ili   kuwezesha kuwezesha tanzania kufanya vizuri katika nyanja ya michezo   katika soko la ndani na nje ya michezo na ulimwenguni. Mhe Lubeleje aliyasema hayo   juzi alipokuwa akifungua Kongamano la Michezo   la vyuo vya ualimu kanda ya kanda linalofanyika katiia chuao cha ualimu   kilichopo Mpwapwa Mkoani Dodoma. Mhe Lubeleje alisema kwa sasa   nchi ya Tanzania inashidwa kufanya vizuri katika nyanja za michezo kutokana na   serikali kushidwa kuwekeza vya kutosha katika sekta hii ya michezo   ambayo inaoneka kukua kwa kasi   hapa nchini. Aidha amesema kwa sasa soko la michezo hapa nchini limeonekana kushika kasi kubwa na   kuwajumuisha vi...

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIKA 30 JELA KWA KOSA LA KULIMA BANGI.

Image
Bwana Odeni Mwikola   akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akisindikizwa kwenda kuanza  Maisha Mapya Jela . Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka thelani jela bwana Oden Mwikola (32) baada ya kupatikana na hatia ya kulima zao haramu la Bangi . Kesi Hizo zilizo kuwa zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal Mayumba wa mahakama Hiyo ya wilaya.  Hakimu mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa Oden Mwikola alitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 11 kifungu kidogo cha 1(a)na(b)ya kuzuia madawa ya kulevya   sura 5 ya mwaka  2015 ambapo walilima shamba la Bangi lenye ukubwa wa  heka moja.  Hata hivyo Mayumba  aliiambia Mahakama kuwa kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi 5 na vielelezo vitatu ikiwemo hati ya ukamataji, maelezo ya onto na taarifa ya mkemia mkuu iliyo thibitisha kuwa mmea ulio patikana Katika shamba la Bwana Odeni ilikuwa ni Bangi.  ...

MPINA WAKULIMA BARUA WAKURUGENZI NCHINI,Walioshidwa kukarabati Majosho.

Image
MPWAPWA KITAIFA /KILIMO NA MIFUGO. Waziri wa mifugo na uvuvi bwana Luhaga Mpina amesema anatarajia kuwaandikia barua za kusudio kuacha kukusanya mapato yote yatokanayo na mifugo kwa Halmashauri zilizo shidwa kutekeleza Agizo lake la azimio la Chato la kukarabati Majosho mabovu ili kuongeza huduma za uogeshaji kwa wafugaji. Waziri Mpina ametoa Agizo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma alipo kuwa kwenye ziara ya kikazi ya kutadhimini zoezi la uogeshaji limefikia Wapi  Tangu lizinduliwe mwezi November mwaka 2018.  Waziri Mpina amesema Katika uzinduzi huo huko Chato alitoa Maagizo manne kwa Halmashauri zote nchini kuyatekeleza kitu alicho kisema kuwa baadhi ya Halmashauri zimetekeleza na zingine hazijatekeleza.  "Nilipokuwa Chato nilitoa maagizo kuwa kila Halmashauri itenge asilimia 15 ya mapato yake ya ndani kwa zitakazo rudi kwa wananchi kuboresha huduma za mifugo nchini. Pia nilisema Majosho yote mabovu yakarabatiwe ili kuongeza fursa za wananchi kuogesha ...