WAZIRI WA MAMNBO YA NDANI YA NCHI ATANGAZA NEEMA KWA BODABODA.
MPWAPWA.
WAZIRI wa mambo ya ndani
ya nchi Mhe George Simbachawene amepiga
marufuku kwa polisi kukamata wananchi,bodaboda
na kuwanyanyasa na pia amepiga marufuku kufanya oparesheni yoyote ndani ya mkoa au
wilaya bila kuwashirikisha wenyeviti wa
kamati za ulinzi na usalama.
Simbachawene ametoa kauli
hiyo wilayani Mpwapwa alipokuwa kwenye ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza
na madiwani wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Simbachawene amesema kuna
baadhi ya polisi wamekuwa wakikiuka
taratibu na kanuni za kipolisi
kwa kuwakamata wananchi na hasa madreva wa pikipiki maarufu kama bodaboda kwa kisingizio kama mimi nimewatuma “ kuanzia
leo kupitia hapa Mpwapwa natangaza bodaboda wasisumbuliwe na kukamatwakamatwa pasipo kuwa na sababu za
msingi” alizungumza .
Pia amewataka bodaboda
wote nchi kuweza kuzingatia sheria za
usalama barabarani ili kuweza kupunguza
ajari na kuweza kuokoa maisha ya wao wenyewe na abiria wao.
Akizungumza na madiwani wa
wilaya ya Mpwapwa amesema madiwani hao
waache kulalamika mbele ya wananchi kwa
utekelezaji wa ilani ya chama cha
mapinduzi waende wakawaonyeshe wananchi
kile walichokifanya hata kama ni kidogo.
“ Ninacho waaambiwa waheshimiwa madiwani tembeeni kifua mbele
acheni kulalamika kwa kileambacho
ulishidwa kutekeleza nenda kaonyeshe
kile ulichotekeleza maana wapo wengine
wamebaki kulalamika tu utafikiri ndo
wamechaguliwa jana kama na matatizo hayawezi yakaisha yote hilo mlifahamu” alisisitiza.
Pamoja na hayo Waziri
Simbachawene amabe pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe amesema
anajifuania utekelezaji wa ilani katika jimbo lake kwa kushirikiana na
madiwani pamoja na watumishi wa serikali alisema tayari nimmeaandaa kitabu cha
kuonyesha kile nilichokitekeleza kwa
wananchi japo kuwa shida haziwezi kuisha zote kwa wakati mmoja.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir
Shekimweri amewataka madiwani hao
kujitadhimini ikiwa imebaki miezi michache
kusitishwa kwa udiwani wao katika sula zima la kuchochea maendeleo katika kata zao .
Shekimweri alisema yapo
maagizo ya kisera ambayo yaliyotolewa lakin baadhi ya kata hazijatekeleza
ikiwemo kila kata kuwa na shule ya sekondari alisema katika kata 33 za wilaya
ya mpwapwa ni kata 9 ambazo hadi sasa hazina
shule za sekondari za kata , pamoja na zahati kila kijiji sasa nawaomba jitadhimini ninyi wenywe au
mkaaianzishe hiyo miradi.
Comments
Post a Comment