Madiwani wa wakumbushwa kujaza tamko la mali pindi udiwani unapokoma.
Mpwapwa.
Waheshimiwa
Madiwani wa Halmashauri yua Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, wamekumbushwa kujaza
za maadili na kuwasilisha Matamko ya
Mali yao na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
pindi Udiwani wao unapokoma mwezi Julai 2020.
Hayo yalisemwa
na Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. George Shilla
wakati akiwasilisha mada ya Tamko la Mali na Madeni katika kikao cha Baraza la
Madiwani la Halimashauri ya Wilaya ya Mpwapwa juzi.
“Jukumu la
kujaza fomu ya maadili ni jukumu la kila kiongozi wa umma na halimuhusu mwajiri wake au mkuu wake wa
idara hivyo kujaza fomu hizi ni takwa la
kisheria ya Maadili namba 13 ya Mwaka 1995 inayomtambua
Kiongozi wa Umma binafsi kila mmoja na sio hiyari ya kiongozi” alifafanua bwana
Shilla.
Aidha Bw.
Shilla alidai kuwa Madiwani wana wajibu wao wa kuwasilisha fomu hizo
kwa Kamishna wa Maadili wenyewe na siyo
kutegemewa kuwasilishiwa na Mkurugenzi wa halmashauri kwani Sheria ya Maadili
namba 13 ya Mwaka 1995 inatambua Kiongozi wa Umma wao binafsi kila mmoja.
Hata hivyo bwana Sshilla
aliwambia madiwani juu ya kuijiepusha na maslahi binafsi kitu alicho kisema kuwa vitendo
vya mgongano wa maslahii umekua na madhara makubwa kwa maendeleo ya taifa na wilaya hivyo
kudidimiza maendeleo ya nchi na wananchi
kukosa imani na viongozi wao.
Kwa upnde
wake makamu mwenyekiti wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa Bwana George
Fuime aliwaomba ofisi ya sekretalieti ya
maadili kuweza kuziwahisha fomu hizo
katika halmasahauri ili wawez kuzijaza kwa wakati.
Pia aliwaomba
sekretalieti ya maadili kufungua ofisi katika wilaya ili kupunguza mlundikano wa watumishi kwenye ofisi za kanda na kuweza kuokoa muda wa viongozi
hao kuwasilisha fomu hizo kwa wakati.
Akijibu hoja
ya ujenzi wa Ofisi za Sekretarieti ya Maadili katika Wilaya ya Mpwapwa, Bw.
Shilla alikili kuwepo changamoto hiyo na
alisema bajeti itaporuhusu ofisi hizo
zitajengwa kila mkoa na hatimaye kila wilaya tofauti na ilivyo hivi sasa ofisi
hizo kupatikana katika Kanda pekee.
Comments
Post a Comment