MPINA WAKULIMA BARUA WAKURUGENZI NCHINI,Walioshidwa kukarabati Majosho.

MPWAPWA KITAIFA /KILIMO NA MIFUGO.

Waziri wa mifugo na uvuvi bwana Luhaga Mpina amesema anatarajia kuwaandikia barua za kusudio kuacha kukusanya mapato yote yatokanayo na mifugo kwa Halmashauri zilizo shidwa kutekeleza Agizo lake la azimio la Chato la kukarabati Majosho mabovu ili kuongeza huduma za uogeshaji kwa wafugaji.

Waziri Mpina ametoa Agizo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma alipo kuwa kwenye ziara ya kikazi ya kutadhimini zoezi la uogeshaji limefikia Wapi  Tangu lizinduliwe mwezi November mwaka 2018. 

Waziri Mpina amesema Katika uzinduzi huo huko Chato alitoa Maagizo manne kwa Halmashauri zote nchini kuyatekeleza kitu alicho kisema kuwa baadhi ya Halmashauri zimetekeleza na zingine hazijatekeleza. 

"Nilipokuwa Chato nilitoa maagizo kuwa kila Halmashauri itenge asilimia 15 ya mapato yake ya ndani kwa zitakazo rudi kwa wananchi kuboresha huduma za mifugo nchini.

Pia nilisema Majosho yote mabovu yakarabatiwe ili kuongeza fursa za wananchi kuogesha mifugo yao kwa urahisi lakini kwa mkoa wa Dodoma ikiwemo Mpwapwa haijakarabati Josho hata moja Sawa na asilimia ."aliongea Waziri Mpina. 

Aidha Waziri Mpina alisema ifikapo mwezi  mwezi Julai mwaka huu watakuwa wamesha tengeneza Kanuni na kuanza kutumika .

Pia amesema agizo lingine ni Kaunda kamati za majosho kote nchini zitakazo ratibu zoez la uogeshaji wa mifugo. 

"Na itakapo fika mwezi July mwaka huu Halmashauri zote ambazo zimeshidwa kutekeleza hayo yote nitawanyang'anya mamlaka ya kukusanya mapato yote yatokanayo na bidhaa za mifugo "Alisisitiza waziri Mpina. 

Naye MKurugenzi wa huduma za mifugo nchini Dkt Hezron Nonga alisema tangu zoezi la uogeshaji lizinduliwe nchini asilimia 56 ya mifugo yote nchini imeogeshwa kwa muda wa miezi mitatu. 

Dkt Nonga amesema mifugo waliogeshwa ni ni Ng'ombe million 19.9,mbuzi million 8.8 Kondoo million 2.88 Punda 224 na  Mbwa 202,900.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.