Walimu wa michezo Nchini wametakiwa kutoa fursa sawa kwa vijana wenye
viapaji wa mjini na vijijini ili kuweza kufikia ndoto zao kimchezo
kama walizofikia wachezaji wakubwa wa kimataifa.
Kauli hiyo ilitolewa na ofisa Elimu Sekondari wilaya ya Mpwapwa
bwana Nelson Milanzi katika zoezi la kufunga kozi ya siku tatu kwa
walimu wa wa michezo wa wilaya ya Mpwapwa.
Mwalimu Milanzi alisema michezo ikiwekwezwa vizuri kwa watoto vijana
inaweza ikapunguza changamoto ya ajira kwa kwa vijana katika taifa
letu “hasa kwa wale wenye vipaji hasa wale walioko pembezoni kwa
mfano akina Mbwana Samata waliotokea mbagala huko mbona hutuwasikii
vijana wenye vipaji wanaotoka vijijini inaamana hawako wenye vipaji
huko sasa nyie nendeni mkawatengeneze akina Samata wengi
”
Naye mkufunzi wa kozi hiyo Bwana Charles Maguzu aliwataka Walimu wa
michezo katika shule za msingi na sekondari kuanza kuipa
kiapumbele michezo katika shule zao kwa lengo la kuibua vipaji na
kuendeleza michezo katika shule zote za msingi na sekondari.
Bwana Maguzu ambae ni mkufunzi kutoka shirikisho la riadha ya dunia
la na afisa michezo wa mkoa wa manyara alidai lengo la kozi hiyo
kuwajengea uwezo walimu kuweza kuwatambua ,kuwaendeleza na kuwalea
wanafunzi wenye viapaji mbalimbali vya kimichezo ili kuweza kufikia
ndoto zao.
Alisema kwa tafiti zilizofanywa na vyama vingi vya michezo katika
nchi zilizo endelea na zinazoendelea zimebaini kuwa michezo pia
hupunguza utoro kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu.
Kwa upande wake afisa michezo wilaya ya Mpwapwa bwana Waziri Lwimbo
alisema kozi hiyo ni utekelezaji wa igazo la Tawala za mkoa na
serikali za mitaa (TAMISEMI) la kuzitaka kila shule kuwa na mwalimu
wa michezo ifikapo 2020 na kozi hiyo ililenga kuwa na walimu 148
lakini walio hudhuria ni walimu 40 tu na alisema lengo la kozi hiyo
ni kuongezea maarifa walimu wa michezo wa mashuleni.
Miongoni mwa walimu waliokuwa kwenye kozi hiyo bwana Awalino Makweta
amelalamikia asilimia kumi zinazotengwa na serikali kwa ajili ya
michezo kuwa hazinufaishi ngazi ya chini bali hunafaisha ngazi ya
wilaya na mkoa kitu alicho kisema kuwa kinawakatisha tamaa walimu
ngazi za chini.
Pia alidai kuwa upungufu maeneo ya michezo na mwamko mdogo wa
wanafunzi na wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika michezo
kunachania kudumaza vipaji vya watoto.
Comments
Post a Comment