AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIKA 30 JELA KWA KOSA LA KULIMA BANGI.
Bwana Odeni Mwikola akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akisindikizwa kwenda kuanza Maisha Mapya Jela .
Mahakama ya Hakimu mkazi
ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka thelani jela
bwana Oden Mwikola (32) baada ya kupatikana na hatia ya kulima zao haramu la
Bangi .
Kesi Hizo zilizo kuwa
zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal Mayumba wa mahakama Hiyo ya
wilaya.
Hakimu mayumba aliiambia
mahakama kuwa mtuhumiwa Oden Mwikola alitenda kosa hilo kinyume na sheria namba
11 kifungu kidogo cha 1(a)na(b)ya kuzuia madawa ya kulevya sura 5
ya mwaka 2015 ambapo walilima shamba la Bangi lenye ukubwa wa heka
moja.
Hata hivyo Mayumba
aliiambia Mahakama kuwa kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi 5 na vielelezo
vitatu ikiwemo hati ya ukamataji, maelezo ya onto na taarifa ya mkemia mkuu
iliyo thibitisha kuwa mmea ulio patikana Katika shamba la Bwana Odeni ilikuwa
ni Bangi.
Pia alisema kutokana na
vielelezo na ushahidi uliopelekwa mahakanani bila Shaka yeyote na
mtuhumiwa alipatikana na hatia . Mtuhuiwa huyo alipo pewa nafasi ya utetezi alikuwa kimya na kuto kueleza chochote.
Katika nafasi ya
maombolezo na ndipo alipo itaka mahakama ipunguzie adhabu kwa kuwa ana majukumu
na familia na watoto 4 wanamtegemea.
Mwendesha mashitaka wa
polisi bwana Stephen Masawa aliiomba mahakama itoe adhabu kwa kwa mtuhumiwa
kutokana na madawa kuwa kero kwa Wananchi na serikali pia na
madhara ya madawa ya kulevya yanayo weza kuadhiri nguvu kazi ya Taifa Pamoja na
kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Katika vita dhidi ya madawa ya kulevya.
Hakimu Mayumba aliambia
mahakama kuwa kwa sasa Bangi imekuwa tatizo Katika jamii yetu na madhara yake
ni makubwa ilipo kuweza kuokoa jamii na kizazi cha badae mtuhumiwa
atafungwa kifungo cha miaka 30 Jela kutokana na vifungu vya sheria namba
11kifungu kidogo 1 (a) na (b) sura ya 5 ya mwaka 2015 ya kuzuia
madawa ya kulevya.
Comments
Post a Comment