DC MPWAPWA AMESEMA HAKUNA MTU ATAKAYE KUFA KWA COVID 19KAMA WATAZINGATIA MAELEKEZO YA WATAALAM.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri Akiongea na Mwandishi wa habari hizi ofisi kwake.
Picha na Mpwapwa Habari.
Na Stephen Noel .
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bwana
Jabiri Shekimweri amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari
dhidi ya ugonjwa wa CORONA CIVID- 19 na
wasitishwe na mamneno ya mitandao juu ya ugonjwa huo.
Mkuu wa wilaya ameyasema hayo jana ofisi
kwake akifanya mahojiani na na mwandishi
wetu juu ya mkakati wa wilaya thidi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo ambao
kwa sasa umekuwa ni janga la kimataifa.
Shekimweri amesema lazima
wananchi waelewe na kuendelea
kuchukua tahadhari thidi ya ugonjwa huo
ambapo kama “ kama wilaya tayari tumesha fanya uhamasishaji katika
makundi yote yanayo tuzunguka wakiwemo
wafanya biasahara bodaboda masokoni
makanisani na misikiti juu ya kujenga uelewa kwa jamii na njia za kujinga na kuwakinga wengine.
Mganga mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Erichard Rwezahura akiwa katika kanisa la Romani Catholic akifundisha wananchi njisi ya kujikinga na corona Hawaonekani pichani,
Pia mkuu wa wilaya hiyo amewataka wananchi
kutafuta taarifa kutoka vyanzo sahihi na
vya kuamninika " acheni kamini mitandao wasikilizeni wataalmu wa faya ili
kuweza kujinusuru”alisisitiza
Tena amewaomba viongozi wa dini ,mila na
kila mmoja kwa imani yake kumlilia mwenyezi Mungu ili atuondolee janga hili la kidunia.
Mganga
mkuu wa wilaya hiyo Dkt Archard Rwezahura alisema kwa kuzingatia maelekezo ya
serikali kupitia waziri mkuu tayari wamesha
tenga maeneo ya kuwahifadhi
wagonjwa hao kama watapatikana na kila
kitu cha afya kimetenga eneo maluum kwa
ajili ya wagonjwa hao kama watapatikana” aliongea Dkt Rwezahura.
Pia Dkt. Rwezahura amesema lazima wananchi wa
wilaya hiyo kuchukua tahadhari pia
lakini wasiwe waoga sana waendelee
kufanya kazi za kimaendeleo huku wakifuatilia maelekezo ya serikali juu ya ugonjwa huo.
"Tukumbuke kuwa Mpwapwa sio kisiwa hvyo
inaingiza wageni wasiopungua 150 kila siku
hivyo lazima tuchukue tahadhari yetu sisi wenywe tunao wahudumia na tunao wapenda " aliongea Dkt
Lwezahura.
Pia mmoja wa wa wanachi wilayani hapo Bi Magreth Boma amesema pamoja na ugonjwa huu kuingia nchini
bado jamii haina uelewa mpana hasa vijijin juu kujikinga hasa kusalimiana Kwa
mikono na wengine wakiamini kuwa wa Afrika hawapati ugonjwa huo.
Comments
Post a Comment