Mwl.Augusta Lupokela kaimu mkurugenzi msaidizi wa mafunzo ya ualimu ,Wizara ya Elimu Sayansi na Tecknolojia.
MBUNGE wa Jimbo la Mpwapwa Mhe George Lubeleje (Seniour MP) ameiomba
serikali kuweza kutenga Bajeti ya
kutosha katika sekta ya michezo nchini ili
kuwezesha kuwezesha tanzania kufanya vizuri katika nyanja ya michezo katika soko la ndani na nje ya michezo na
ulimwenguni.
Mhe Lubeleje aliyasema hayo juzi alipokuwa akifungua Kongamano la
Michezo la vyuo vya ualimu kanda ya
kanda linalofanyika katiia chuao cha ualimu
kilichopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Mhe Lubeleje alisema kwa sasa nchi ya Tanzania inashidwa kufanya vizuri
katika nyanja za michezo kutokana na
serikali kushidwa kuwekeza vya kutosha katika sekta hii ya michezo ambayo inaoneka kukua kwa kasi hapa nchini.
Aidha amesema kwa sasa soko la michezo hapa nchini
limeonekana kushika kasi kubwa na kuwajumuisha vijana wengi na hivyo kwa kuona
umuhimu huo serikali ya awamu ya tano imeamua kurudisha tena michezo katika vyuo ili kuweza kupata vijana wenye viapaji vya michezo lakini pia kuwapata
walimu watakao weza kufundisha michezo katika ngazi ya shule za msingi na sekondari.
“ Kwa kweli kwa sasa Tanzania bado hatauajafanya
vizuri katika mashindano ya michezo hapa nchini llakini yote hayo inatokana na
serikali kushidwa kuwekeza vya kutosha
kwenye sekta ya michezo ikiwemo bajeti, miundo mbinu pamoja na
vifaa vya michezo sasa nitajitahidi kushawishi bungeni ili serikali iweze kutenga bajeti ya kutosha katika sekta hii ambayo kwa sasa imebeba
ajira kubwa ya vijana wetu” aliongea Lubeleje.
Kwa Uapnde wake
Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa
mafunzo ya ualimu kutoka wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia Bi Augusta
Lupokela alisema alisema kuwa
Chombo hicho kiliocho anzishwa miaka sabini iliopita kikiwa na lengo la
kusimamia michezo katika shule za
sekondari na msingi kwa lengo kuweza kufanya vizuri katika ngazi ya Taifa na ulimwengu mzima .
Hata hivyo
amesema kuwa chombo hicho kilifungwa zaidi ya miaka 20 baada ya serikali kufuta
michezo katika vyuo vya ualimu lakini
alisema “ kwa mimi kama mwanamichezo pia
naona fahari sana kuwa michezo imerudi
tena nikiwa madarakani lakini lakini
lengo kuu ni kuendeleza michezo katika ngazi ya sekondari na shule za
msingi hivyo lazima tufanye kwa tija ili
tuweze kupata wanamichezo mahiri watakao weza kitangaza Tanzania katika
ulimwengu wa michezo na Afrika mashariki.
Amesema UMISAVUTA
pia ilikuwa pia kuwafunza zaidi
walimu kimwili kiakili kitaaluuma na kimalezi yanaweza kumtambulisha
mtanzania popote atakapo kuwapo.
Pia amesema malengo mengine ilikuwa kuratibu na kupima
michezo ya sanaa katika vyuo vya ualimu
Tanzania ili kuweza kubaini ipaji vya walimu katika vyuo na kuendeleza sera ya michezo na sanaa katika jamii ya Kitanzania .
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa vyuo vya
aulimu kanda ya Kati mkuu na chuo cha ualimu Kinamapanda
Mwl , Maulidi Hamisi amesema pamoja na serikali kurudisha
michezo vyuoni lakini bado shule za msingi na vyuo vinakabiliwa na
changamoto kubwa ya maeneo ya pamoja na vifaa vya michezo , ambazo alisema
vinaweza kutishia uendelevu wa michezo vyuoni .
Aidha Mwl. Maulidi ametumia fursa hiyo kuiomba serikali na wadau wa michezo kote nchini kuweza
kuweza kusaidia kauapatika na kwa vifaa vya michezo
na serikali kuweza kutenga maeneo ya michezo kwa ajili ya kuendeleza michezo hapa nchini .
Kongamano hilo
la siku nne ambalo limejumuisha vyuo vya ualimu Kinampanda , Bustani NA Chuo
cha ualimu Mpwapwa na mashinda kitafaifa
yatanyika Mkoani Lindi baada ya kila kanda kupata timu moja itakayo wakilisha kanda.
Comments
Post a Comment