Posts

Image
Mwl.Augusta Lupokela kaimu mkurugenzi msaidizi wa mafunzo ya ualimu ,Wizara ya Elimu Sayansi na Tecknolojia. MBUNGE wa Jimbo la Mpwapwa   Mhe George Lubeleje (Seniour MP) ameiomba serikali kuweza   kutenga Bajeti ya kutosha    katika sekta ya michezo   nchini ili   kuwezesha kuwezesha tanzania kufanya vizuri katika nyanja ya michezo   katika soko la ndani na nje ya michezo na ulimwenguni. Mhe Lubeleje aliyasema hayo   juzi alipokuwa akifungua Kongamano la Michezo   la vyuo vya ualimu kanda ya kanda linalofanyika katiia chuao cha ualimu   kilichopo Mpwapwa Mkoani Dodoma. Mhe Lubeleje alisema kwa sasa   nchi ya Tanzania inashidwa kufanya vizuri katika nyanja za michezo kutokana na   serikali kushidwa kuwekeza vya kutosha katika sekta hii ya michezo   ambayo inaoneka kukua kwa kasi   hapa nchini. Aidha amesema kwa sasa soko la michezo hapa nchini limeonekana kushika kasi kubwa na   kuwajumuisha vi...

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIKA 30 JELA KWA KOSA LA KULIMA BANGI.

Image
Bwana Odeni Mwikola   akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akisindikizwa kwenda kuanza  Maisha Mapya Jela . Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka thelani jela bwana Oden Mwikola (32) baada ya kupatikana na hatia ya kulima zao haramu la Bangi . Kesi Hizo zilizo kuwa zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal Mayumba wa mahakama Hiyo ya wilaya.  Hakimu mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa Oden Mwikola alitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 11 kifungu kidogo cha 1(a)na(b)ya kuzuia madawa ya kulevya   sura 5 ya mwaka  2015 ambapo walilima shamba la Bangi lenye ukubwa wa  heka moja.  Hata hivyo Mayumba  aliiambia Mahakama kuwa kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi 5 na vielelezo vitatu ikiwemo hati ya ukamataji, maelezo ya onto na taarifa ya mkemia mkuu iliyo thibitisha kuwa mmea ulio patikana Katika shamba la Bwana Odeni ilikuwa ni Bangi.  ...

MPINA WAKULIMA BARUA WAKURUGENZI NCHINI,Walioshidwa kukarabati Majosho.

Image
MPWAPWA KITAIFA /KILIMO NA MIFUGO. Waziri wa mifugo na uvuvi bwana Luhaga Mpina amesema anatarajia kuwaandikia barua za kusudio kuacha kukusanya mapato yote yatokanayo na mifugo kwa Halmashauri zilizo shidwa kutekeleza Agizo lake la azimio la Chato la kukarabati Majosho mabovu ili kuongeza huduma za uogeshaji kwa wafugaji. Waziri Mpina ametoa Agizo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma alipo kuwa kwenye ziara ya kikazi ya kutadhimini zoezi la uogeshaji limefikia Wapi  Tangu lizinduliwe mwezi November mwaka 2018.  Waziri Mpina amesema Katika uzinduzi huo huko Chato alitoa Maagizo manne kwa Halmashauri zote nchini kuyatekeleza kitu alicho kisema kuwa baadhi ya Halmashauri zimetekeleza na zingine hazijatekeleza.  "Nilipokuwa Chato nilitoa maagizo kuwa kila Halmashauri itenge asilimia 15 ya mapato yake ya ndani kwa zitakazo rudi kwa wananchi kuboresha huduma za mifugo nchini. Pia nilisema Majosho yote mabovu yakarabatiwe ili kuongeza fursa za wananchi kuogesha ...

LUFU WAPATA BARABARA TANGU UHURU.

Image
SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma   imewataka wakazi wa kata za Mwanawota na Lufu   waliopatiwa fedha za ukarabati   wa barabara kuthaminisha ukabarabati wa barabara hizo   sambamba na uboereshaji uchumi wa kata zao kwa kufanya kazi kwa Bidii. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa   Jabir Shekimweri alipotembelea   barabara hizo kwa ajili ya kuangalia hali halisi ya ukarabati unaoendelea   katika kata hizo chiniya wakala wa barabara Vijijini TARURA Wilaya ya Mpwapwa. Barabara zilipatiwa fedha za ukarabati   ni barabara ya kibakwe ,Mwanawota yenye urefu wa kilometa 16 yenye dhamani ya shilingi shilingi milion 713,000,000/= na barabara ya kata ya Rufu yenye urefu   wa kilometa   kilometa 16 pia Shekimweri alisema   hakuna zaidi kwa kata hizi kutoa shukrani kwa serikali   ya awamu ya tano zaidi ya kupandisha kiwango cha uchumi katika kata zao   ambazo zimepatiwa fedha za ukarabati. “...

UHARIBIFU WA MAZINGIRA WATISHIA JAGWA.

Image
  Baadhi ya akina mama wakipanda mti katika kata ya Mazae KUFUTIA uharibifu mkubwa wa mazingira   unaofanywa na watu katika   wilaya ya   Mpwapwa   kunatishia   kupungua kwa   upatikanaji wa   huduma ya maji   kwa baadhi ya vijiji vya wilaya ya Mpwapwa. Hali hiyo imetanabaishwa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri kwenye   kilele cha siku ya   mazingira   duniani iliyofanyika katika kijiji cha Idilo kata ya Mazae. Shekimweli amesema   uhai na ustawi wa wa   Taifa letu unategemea   sana   mazingira   yanayotuzungunguka   hivyo alisema uharibifu wa mazingira   ni moja   kati   ya tishio   kubwa la uhai wa binadamu na viumbe vingine   vinavyo tegemea mazibgira   katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Aidha Shekimweri amesema   mabadiliko ya   ya tabia   ya nchi   sasa   yamekuwa ni tishio   la us...

PAROKO KANISA KATOLIKI ATAKA HUDUMA ZA JAMII KUBOREKA MPWAPWA.

Image
Paroko wa kanisa Katoliki Parokia ya Mpwapwa  Pd Daud Ngimba  akihubiri anisani . PAROKO wa kanisa katoliki Parokia ya Bikira Maria wa Fatima Mpwapwa jimbo   kuu la Dodoma Padre Daud Ngimba imeitaka jamii ya   watu wa Mpwapwa na viongozi wa Serikali   kuweza kutumia fursa ya Serikali kuhamia Mkoani Dodoma   kuboresha huduma za kijamii kama ,   Barabara,shule , Afya na huduma za maji   wilayani hapo. Padre Ngimba aliyasema   hayo mwishoni mwa wiki    alipo kuwa akitoa mahubiri   kwenye Misa ya   Utatu mtakatifu   na alipokuwa akiutambulisha mkakati wa kanisa hilo katika kujikita katika utatuzi wa changamoto zinazo ikabili jamii ya Mpwapwa. Padre   Ngimba alisema wakristu ,Tasisi za dini    pamoja na serikali za mitaa katika mkoa wa Dodoma   zitaweza kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuhamisha makao makuu ya serikali kuja Dodoma n...

DARAJA LA GODEGODE LITAFIFISHA MAPATO YA HALMASAHAURI.

WANANACHI wa kata ya Godegode,Pwaga na Lumuma wameiomba serikali kuweza   kurudisha mawasiliano   ya barabara    baada ya   daraja   la Godegode   ambalo ni kuungo muhimu kati ya kata hizo   na makao makuu ya wilaya   kusomwa na maji   katika msimu   wa mvua mwaka huu. Wanachi wa   kata   hiyo   wametoa   ombi hilo mbele ya naibu waziri wa ujenzi   Mhe Eliasi Kuandikwa (MB) alipokuwa kwenye   ziara   ya   kukakuga ujenzi wa barabara za Mpwapwa na kufika katika   daraja hilo   kuangalia   hali harisi ya   changamoto ya   usafiri katika eneo hilo. Diwani wa kata ya godegode Bwana Tanu Makanyago amesema daraja hilo ambalo ndio muhimili   mkuu wa   mawasiliano kati ya   kata ya Godegode,Pwaga, na Lumuma kwa mawasiliano . Aidha Bwana Mkanyago  amesema kutokana na uharibifu   wa daraja hilo   kumepelekea maisha ya watu wanaois...