LUFU WAPATA BARABARA TANGU UHURU.
SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imewataka wakazi wa kata za Mwanawota na Lufu
waliopatiwa fedha za ukarabati wa barabara kuthaminisha ukabarabati wa
barabara hizo sambamba na uboereshaji
uchumi wa kata zao kwa kufanya kazi kwa Bidii.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri alipotembelea barabara hizo kwa ajili ya kuangalia hali
halisi ya ukarabati unaoendelea katika
kata hizo chiniya wakala wa barabara Vijijini TARURA Wilaya ya Mpwapwa.
Barabara zilipatiwa fedha za ukarabati ni barabara ya kibakwe ,Mwanawota yenye urefu
wa kilometa 16 yenye dhamani ya shilingi shilingi milion 713,000,000/= na
barabara ya kata ya Rufu yenye urefu wa
kilometa kilometa 16 pia
Shekimweri alisema hakuna
zaidi kwa kata hizi kutoa shukrani kwa serikali ya awamu ya tano zaidi ya kupandisha kiwango
cha uchumi katika kata zao ambazo
zimepatiwa fedha za ukarabati.
“Haiwezekani barabara zinapendeza zinanga’aa lakini bado
uchumi unakuwa chini hivyo viongozi kata
na chama mjipange sasa vizuri kwa miundo
mbinu hii barabara iendane na viwango vya kukua kwa uchumi kuboresha huduma za jamii kama elimu afya na uchumi.” aliongea.
Shakimweri alisema serikali imetoa zaidi ya billion na milion miatano kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizi ikiwa
nalengo la kufungua fursa za kata hizi kiuchumi,kielimu na huduma za jamii..
Meneja wa wakala wa barabara vijijini TARURA Wilaya ya
Mpwapwa Mwandisi Godfrey Nkinga alisema kutokana na kukamilika kwa barabara hizo kutafungua fursa nyingi katika kata husika
ikiwemo kuboreka kwa huduma za jamii, pamoja na kukuza uchumi wa kata husika
kwa kuweza kusafirisha mazao yao kirahisi au wanunuzi kufuata bidhaa hadi
kijijini.
Mwandisi wa wa
anayesimamia ujenzi wa barabara ya Wota hadi Mwanawota Mwandisi Malisa
balingumu MATHIAS Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni JP Traders alisema ukarabati huo unatarajiwa kukamilika kabla ya
july 27 mwaka huu na ukarabati huo unakadiliwa kutumia jumla ya shilingi milioni 783,000,000/=ambapo
alisema mpaka ukarabati umefikia asilimia 40 ya kazi yote.
Naye Mwandishi anayejenga barabara ya Kidege LUFU
mwandisi Malisa Daniel wa Kampuni ya Classic Buld(LGS) LTD alisema
barabara hiyo ilikuwa haijakarabaitiwa
tangu uhuru na hivyo ilikuwa
inawalazimu wananchi wa kata hiyo hiyo kutumia Punda kusafirishia mizigo
yao au kama kuna mgonjwa walikuwa
wanambeba kwenye vitanda ili kufikia huduma za barabara.
Alisema ujenzi wa huo
ni mpango serikali wa kuunganisha vijiji vyote kuwa una
uhakika wa barabara za uhakika zinazopitika msimu mzima.
Kata za LUFU na Mwanawota wilayani Mpwapwa ni miongoni kata kongwe hapa wilayani zinazotegemewa kwa uzalishaji wa mazao ya Mahindi, Maharagwe,
na mbogamboga ambazo zinaweza kulisha
mkoa mzima wa Dodoma na wilaya zake.
Comments
Post a Comment