PAROKO KANISA KATOLIKI ATAKA HUDUMA ZA JAMII KUBOREKA MPWAPWA.
Paroko wa kanisa Katoliki Parokia ya Mpwapwa Pd Daud Ngimba akihubiri anisani .
PAROKO wa kanisa katoliki Parokia ya Bikira Maria wa Fatima
Mpwapwa jimbo kuu la Dodoma Padre Daud
Ngimba imeitaka jamii ya watu wa Mpwapwa
na viongozi wa Serikali kuweza kutumia
fursa ya Serikali kuhamia Mkoani Dodoma kuboresha
huduma za kijamii kama , Barabara,shule
, Afya na huduma za maji wilayani hapo.
Padre Ngimba aliyasema
hayo mwishoni mwa wiki alipo
kuwa akitoa mahubiri kwenye Misa ya Utatu mtakatifu na alipokuwa akiutambulisha mkakati wa kanisa
hilo katika kujikita katika utatuzi wa changamoto zinazo ikabili jamii ya
Mpwapwa.
Padre Ngimba alisema
wakristu ,Tasisi za dini pamoja na
serikali za mitaa katika mkoa wa Dodoma
zitaweza kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuhamisha
makao makuu ya serikali kuja Dodoma na kuipandisha hadhi mkoa wa Dodoma
kuwa kuwa jiji kwa kuboresha huduma za
jamii na kuyapatia majawabu maswali ya
changamoto zilizopo katika mkoa huo kwa
wananchi wanao waongoza kwa vitendo.
Aidha Padre Ngimba alisema kuwa wilaya nyingi za Jiji la
Dodoma ninakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za utenadaji wa
mazoea,migogoro na usimamizi duni wa
shughuli za serikali ikiwamo mazingira “kwa sasa ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa
na chanagamoto za kielimu kwa kuwa na ufaulu duni, ubovu wa miundo mbinu uchahache wa hospitali za binafsi ,pamoja changamoto
za huduma za maji vijijini ”aliongea .
Pia alisema viongozi wa kuchaguliwa kwa kushirikiana na watendaji
wa Halmashauri kuweza kuboresha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami barabara ya Mbabe –Mpwapwa
wenye urefu wa kilometa 60 ili kuweza kuchochea
maendeleo ya Mpwapwa kwa kuwekeza
katika sekta ya usafiri pamoja na viwanda.
Pdre Ngimba alisema
watu binafsi ,tasisi za dini lazima ziwe sehemu za utatuzi wa changamoto
zinazo ikabili jamii ya watu wa Mpwapwa kwa kuwekeza
katika shughuli za maendeleo.
Hata hivyo alisema “ Mpwapwa ni miungoni mwa wilaya inayo
kabiliwa na changamoto nyingi kama
kanisa lazima tuwe sehemu ya utatuzi wa changamoto hizo kwa kuwekeza katika sekta ya elimu afya na huduma jamii”aliongea
Padre Ngimba.
Alisema katika mkakati wa kanisa ndani ya miaka mitano wataweza kujenga shule ,Zahati
na kuchimba kisima cha maji amabacho
kitaweza kupunguza adha ya wananchi kutafuta maji mbali hasa kipindi cha kiangazi.
Comments
Post a Comment