UHARIBIFU WA MAZINGIRA WATISHIA JAGWA.
Baadhi ya akina mama wakipanda mti katika kata ya Mazae
KUFUTIA uharibifu
mkubwa wa mazingira unaofanywa na watu
katika wilaya ya Mpwapwa
kunatishia kupungua kwa upatikanaji wa huduma ya maji kwa baadhi ya vijiji vya wilaya ya Mpwapwa.
Hali hiyo
imetanabaishwa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri kwenye kilele cha siku ya mazingira
duniani iliyofanyika katika kijiji cha Idilo kata ya Mazae.
Shekimweli amesema uhai na ustawi wa wa Taifa letu unategemea sana
mazingira yanayotuzungunguka hivyo alisema uharibifu wa mazingira ni moja
kati ya tishio kubwa la uhai wa binadamu na viumbe vingine vinavyo tegemea mazibgira katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
Aidha Shekimweri amesema mabadiliko ya
ya tabia ya nchi sasa
yamekuwa ni tishio la usalama wa mataifa
kama ilivyo kwa ugaidi na vita .
Amesema katika nchi za
wenzetu kama visiwa vya Maldives ambako mabadiliko ya
ya nchi yanatishia kuvifuta
visiwa hivyo katika ramani ya Dunia
kutokana na kuongezeka na kupanda
kwa kina cha Bahari”
aliongea Shekimweri
Hata hivyo Shekimweri
amewataka maofisa mazingira wote wilayani kuweza kueneza elimu na teknolojia ya matumizi wa nishati mbadala kuliko kubaki
kuitangaza kama nadharia na elimu hiyo
kuwa mjini na kuwaacha watu wa vijijini ambao ndio kundi kubwa linalo husika
katika katika matumizi na uzalishaji wa
nishati ya mkaa na kuni.
Diwani wa kata ya Mazae
Mhe Wiliam Vahae aliomba serikali kuweza kubadilisha
sheria ya ya kutoza faini au kuwanyima msamaha watu wote wanapatikana na
hatia za uharibifu wa mazingira kutokana
na na madhara yatokanayo na uharibifu wa mazngira kwa sasa.
.
Kwa upande wake Ofisa
mazingira wa wilaya ya Mpwapwa Bwana
Teodory Mlokozi amesema kuwa kuwamadhumuni
ni kuhamasisha jamii na duniani
kuweza kuelewa masuala yanayo husu hatua za kuhifadhi mazingira na kutoa fursa kwa jamii kufahamu
kwamba jamii ina wajibu wa kuzuia
madhara na mabadiliko hasi
katika mazingira na kufurahia
yao na vizazi vijavyo.
Pia amesema Mpwapwa ni
miongoni mwa wilaya ambayo haiku vizuri katika utunzaji wa mazingira hivyo ametumia fursa hiyo kuwataka wanajamii kuweza kutoa taarifa za watu wanao husika katika
uharibifu wa mazingira.
Comments
Post a Comment