DARAJA LA GODEGODE LITAFIFISHA MAPATO YA HALMASAHAURI.
WANANACHI wa kata ya Godegode,Pwaga na Lumuma wameiomba
serikali kuweza kurudisha
mawasiliano ya barabara baada ya
daraja la Godegode ambalo ni kuungo muhimu kati ya kata
hizo na makao makuu ya wilaya kusomwa na maji katika msimu wa mvua mwaka huu.
Wanachi wa kata hiyo
wametoa ombi hilo mbele ya naibu
waziri wa ujenzi Mhe Eliasi Kuandikwa
(MB) alipokuwa kwenye ziara ya
kukakuga ujenzi wa barabara za Mpwapwa na kufika katika daraja hilo
kuangalia hali harisi ya changamoto ya
usafiri katika eneo hilo.
Diwani wa kata ya godegode Bwana Tanu Makanyago amesema daraja hilo ambalo ndio muhimili
mkuu wa mawasiliano kati ya kata ya Godegode,Pwaga, na Lumuma kwa
mawasiliano .
Aidha Bwana Mkanyago amesema kutokana na uharibifu wa daraja hilo kumepelekea maisha ya watu wanaoishi katika
kata hizo kupanda bei kwa gharama maisha
ikiwemo usafiri,bidhaa madukani lakini pia kuchukua muda mrefu kwa kuyafikia
makao makuu ya wilaya.
Chihimba amesema Chanzo cha Madaraja hayo kusobwa na maji ni
uharibifu mkubwa wa mazingira
unaoendelea katika milima, amabapo watu huendesha shughuli za kibinadamu katika vilele vya milima na hivyo kusababisha
maji kutiririka na kwa kasi kwenye madaraja na hivyo kupelekea madaraja kuvunjika .
Mwananchi Mwingine aliyejitambulisha kwa jina Mwl,Fustine Valelian alisema
kutokana na kuvunjika kwa daraja hilo
kunatishia pia maisha ya akina mama wajawazito na wagonjwa pindi
apatikanpo mgonjwa wa dharula na hivyo hupelekea kuzunguka sana
na hivyo kutishia usalama wa wagonjwa.
Tena ameongeza kuwa endapo daraja hilo halitajegwa kwa wakati pia kunatishia halmashauri kukosa mapato ya ndani yanayo tokana na mazao
hasa kipindi hiki cha msimu wa
mavuno kwa “maana magari hayatapita tena mpwapwa yatazungukia Lumuma na kutokea
kilosa hivyo daraja hili ni muhimu kwa
maendeleo ya halamsahauri,
kiuchumi,kijamii kisiasa pia”aliongea
Mwl Faustine.
Kwa upande wake
Naibu waziri wa wa ujenzi
Mhe Elias Kuandikwa (MB)
alisema kuwa serikali imejipanga
kujeresha mawasiliano hayo yaliyokuwa wamekatika na
wananchi hao kuendelea kupata huduma kama awali .
Naibu Waziri alisema “ Kwa sasa natambua adha mnayo
ipata mala baada ya daraja hili kukatika
lakini serikali yenu ni sikivu na
hivyo inajitahidi kurejesha mawasiliano
mala moja ili kuweza kuwaondolea adha
hii hata kwa fedha za dharula”aliongea
Mhe ,Kuandikwa.
Hata hivyo Naibu
waziri alisema kuwa changamoto iliyo kuwapo ni kwamba
serikali ilipanga bajeti kidogo lakini kutokana na uharibifu mkubwa wa uliosababishwa na mvua
uliongeza gharama ujenzi wa daraja hilo.
Mhe, Kuandikwa liwataka
wananchi kata ya Godegode kuweza kuhifadhi na kutunza mazingira ili kuweza
kutunza miundo mbinu ya
seriakali iliyopo na inayotarajiwa
kujenga katika maeneo hayo ikiwemo Reli
ya mwendo kasi inayotarajiwa kupita katika kata ya Godegode.
Comments
Post a Comment