UFISADI WA KUTISHA MAPATO HALMASHAURI YA MPWAPWA
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma bwana Jabir Shekimweri
amewapa masaa 6 ya kujieleza kwa barau kwa watendaji wa kata na
vijiji kutokana kuto wasilisha fedha za mapato ya ndani jumla ya
shilingingi milioni 84,202500/=kama mapato ya mwezi January
.
Shekimweri ametoa agizo hilo katika kikao cha baraza la madiwani
kilicho fanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa halmasahauri.
Shemweri kuna dalili za udanganyifu mkubwa ulipo kwa watendaji wa
halmasahauri na watendaji wa kata katika ukusanyaji wa mapato kwa
kutumia mfumo maluumu wa mashine zijulikanazo kama POS.
Aidha Shekimweri amedai serikali ikiwa katika harakati za kuboresha
mapato kuimarisha uchumi wa wilaya kuna baadhi ya watendaji wa
serikali wasio waaadilifu bila uwoga wamekuwa wakihujumu mapato ya
halmashauri hiyo na kuifanya halamasahuri hiyo kuto kusonga mbele.
“Ikiwa kama Ilani yetu ya kusimamia uwajibika ,uadilifu na utenadaji
bora wakazi kuna baadhi ya wenzetu wakiwamo watendaji wa kata na
vijiji na watumishi wakihujumu mapato yetu na halamasahauri na
kuifanaya halmasahauri isisinge mbele nawaaambia hii jinai kama kweli
mtu akibainika katika hili baada ya kujilidhisha hatua za kisheria na
kinidhamu zitamwandama”aliongea Shekimweri.
Shekimweri alisema kufuatia hali hiyo tayari amemwagiza mtaalamu wa
mifumo ya kukusanyia mapato kutoka TAMISEMI kuja kufanya uchunguzi wa
kina katika mfumo huo ili kubaini hasara zaidi ambayo kwayo
imesabaisha watendaji na watumishi wa halmashauri
.
Alisema pia kuna udanganyifu mkubwa katika ukusanyaji wa ushuru wa
ushuru wa samaki katika bwawa la mtera kunakosababisha uadlifu wa
watendaji na mfumo wa hlamsahauri wa ukusanyaji wa mapato hayo.
Mwenyekiti wa halamashauri hiyo bwana Donart Ngwezi alisema baada kuto
ridhishwa na ukusanyaji na taarifa za mapato zinazo wasilishwa kwenye
kamati yake ya uchumi mipango na fedha aliamua kuunda timu ndogo ya
kujiridhisha na kuzungukia katika baadhi ya vyanzo vya mapato likiwamo
bwawa la mtera katika mwalo wa chungu ambapo alisema ndani ya siku nne
waliweza kukusanya kiasi cha shilingi milion 7,090,200/=wakati
watenadaji kwa mwezi walikuwa wanawasilisha shingi milion 2,800,000
hadi milion 3,000,000/=.
Hata hivyo alisema baada ya kuchunguza katika mfumo wamebaini ufisadi
mkubwa wa mapato ya halmasahauri hiyo katika mashene za kukusanyia
ushuru huo ambao umeisababishia halmasahauri jumla ya shilingi
milioni 84,202,500/=kwa mwezi desemba na January.
“tulipo angalia kwenye mfumo tulibaini uwizi mkubwa uliofanywa na
watendaji hao kwa mfano kwenye mashine namba301500010172 kwa mwezi
januri ilikusanya jumla ya shilingi milion 45,889,900/=lakini
zilizowekwa banki 1,710,500/=mashine inayo ishia namba 2830 ilikusanya
jumla ya milion 2,514,000/iliyo wekwa benki 164,300 mashine yenye
namba 0181 ilikusanya shilingi 35254000/= zilizowekwa banki ni
shilingi 974,000/=”aliongea Nghwezi.
Aliongeza kusema “ katika mashine namba 2628 ilikusanya jumla ya
shilini milioni 4,355,810 pesa iliyo wekwa banki ni shilingi
518,000/= alisema katika mashine namba 2826 ilikusanya jumla ya
shilingi 4,167,500/=pesa iliyo wekwa benki ilikuwa ni shilingi
194,000/= kwa jumla ya mapato yalikuwa milion 92,181,300 akini zilizo
enda benki zilikuwa milion 7,978,800 alifafanua .
Nghwenzi alisema kuwa srikali ya awamu ya tano ikiwa inasisitiza
uadilifu kwa watenadaji lakini baadhi ya watendaji wa Mpwapwa hawana
uwoga kabisa na kuibia hadi kwenye mfumo hivyo baada ya watalaamu wa
mifumo kutoka Tamisemi kubaini haya tutachukua hatua kwa wote watakao
husika."alisisitiza
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmasahauri hiyo alikanusha
kuwa kuna uwizi uliofanyika bali alisema kuwa kuwa kamati hiyo
imeschukua takwimu na risiti zilizo kuwa zimekosewa na hivyo bado
zinasoma kwenye mfumo.
Alisema kuna “baadhi ya watendaji ambao wamekuwa wakikosea tarakimu
baada ya kuandika laki mbili anaweza anadika milioni mbili milion
mbili anaweza kuandika milioni ishirini lakini kwa vile watalaamu
kutoka tamisemi wamefika hivyo watabaini mapungufu au uwizi kama upo”
aliongea Maje.
Baada ya mkutano kuisha Mkuu wa wilaya hiyo alitaka kuanza kufanya
mahojiano na watenaji wa kata ya Pwaga,Mpwapwa mjini na Mtera,
Comments
Post a Comment