MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU WATUMISHI HEWA.
SERIKALI imetangaza msimamo wake kwa watumishi ambao walibainika
kuwa na vyeti feki na wale wasiokuwa na vyeti vya kidato cha nne kuwa hawana
madai yoyote ya kuidai serikali baada ya Rais John Magufuli kutangaza kufanyika
kwa uhakiki kwa watumishi wa umma.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa idara ya uendelezaji sera,
Mathias Kabundugulu,wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi cha kujadili
masuala ya utawala na rasilimali watu kwa mamlaka za serikali za mitaa, wizara
na mikoa.
Amesema watumishi ambao wamebainika na kuondoka wenyewe,
wamefutwa kwenye orodha ya watumishi wa umma na hawana madai wanayodai
serikalini huku amesema pamoja na zoezi hilo kukamilika kwa muda ambao
umepangwa, wapo baadhi ya maafisa utumishi wameendelea kuwafumbia macho watu
wasiokuwa na vyeti vya kidato cha nne.
Naye katibu mkuu wa wizara ya Tamisemi, Mhandisi Mussa Iyombe,
amesema kumekuwepo na changamoto mbalimbali zinazofanywa na maafisa wa utumishi
katika halmashauri mbalimbali nchini.
Selemani Jafo ni Waziri wa nchi, ofisi ya rais, tawala za mikoa
na serikali za mitaa, Tamisemi, , amewataka makatibu wakuu wa wizara yake na
wale wa ofisi ya rais utumishi, kuangalia upya miongozo na sheria ambazo
zimekuwa kandamizi kwa watumishi wa umma.
MWISHO
Comments
Post a Comment