TANZANIA YA KESHO INATISHIWA NA WIMBI LA WATOTO WA MITAANI.




IMEELEZWA kuwa  tunaweza kuitengeneza Tanzania ya kesho kwa kuwekeza  katika masalahi mapana ya watoto kimaadili,kiuchumi ,kielimu.
Kauli  hiyo ilitolewa na  mkurugenzi mtendaji wa kituo  cha kompasheni namba TZ 236 KKKT  bwana Mboka Mwaipopo alipkuwa akiongea na waaandishi wa habari  ofisi kwake  hivi karibuni.
Bwana Mboka alisema kuwa kumekuwako na vituo hivyo vilivyo anzishwa chini ya makanisa  vikiwa na lengo la kuwalea watoto katika Nyanja za kielimu, kiroho na  kiuchumi ili  waweze kuwa wazalishaji na   kuwezesha kuifikia Tanzania viwanda .
Aidha Mboka alisema  kuwa siku zinavyo zidi  kusonga mbele kuna kunazidi kuongezeka kwa watoto wanaojulikana kama watoto wa mitaani kitu alicho kisema kuwa kinatishia ustawi wa taifa lolote siku za mbeleni.
“Hiki ni kizazi cha watanzania wa Tanzania ya  kesho tukiendelea kuwaita watoto wa mitaani  tutambue kuwa Tanzania ya kesho nayo itakuwa ya mitaani kwa sabubu hii ndio picha ya Tanzania ya Kesho ,hivyo lazima tujitoe sote kwa kuunganisha nguvu tukiwalea watoto hawa kimaadili,iuchumi na kielimu ili kuweza kuifikia Tanzania tunayoitaka”aliongea Bwana Mboka.
Mboka alisema  katika kutuo chake Namba 236 chenye watoto 239 kimeweza kuwasiadia baadhi ya watoto kufukia ndoto zao za kimasomo japo wengi wao walikuwa wamekata tama ya kusoma tena na wengine walisha anza kujiingiza kwenye masula yasiyo kuwa  ya msingi na tija kwa jamii na watoto.
Hata hivyo mboka alitumia fursa hiyo  kuiomba serikali kuongeza ushirikiano  zaidi  kwa vituo hivyo nchi nzima ili kuweza kufanikisha  ndoto za watoto hao  kuweza kuwapatia haki zao za msingi  za kimalezi,kielimu na mazingira rafiki ya kuishi,
Pia mboka aliongeza kusema kuwa shughuli wanazozifanya katika vituo hivyo ni malezi,kuwapa watotoo chakula,masomo na baadhi yao wenye mazingira hatarishi kabisa kujengewa nyumba  za kuishi.
Akitaja chanagamoto zinazo wazunguka Mkurugenzi huyo bwana Mboka  alisema  kuwa changamoto za mimba za utotoni ni kikwazo kinacho ikabili kituo hicho kuwa baadhi  vijana huwarubuni watoto hao  huwapa mimba na kuwatelekeza ,
Alisema  kwa miaka mwili ya 2016-2017 jumlaya mabinti 7 walipewa ujauzito  na wengine waliachishwa masomo na hivyo kufifisha ndoto zao na ufadhili ulikoma.
Kwa upande wake mmoja wa watoto walioweza kunufaika na mpango huo Anna Makochoalisema kuwa  katika vituo hivyo kuna malezi ambayo kuwa  huwajenga kuwa wazalishaji,watu wema na wabunifu katika maisha ili waweze kupambana na mazungira yanayo wazunguka katika ajira.
Anna  alisema kuwa wazazi na walezi wasikate tamaa na kuwachia  watoto wao kuwalea na kuwaacha wakijilea wao  na hivyo kupelekea kushidwa kuwa vijana wazalishaji .


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.