JAFFO ATOA MIEZI MINNE KWA WATUMISHI IDARA YA MAJI.
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo ametoa miezi minne
kwa mamlaka zote za maji nchini kuhakikisha zinafunga dira za maji kwa wateja
wake wote kwa asilimia 90 na kuwa na miundombinu ya kutibu maji watakaoshindwa
kufikia hapo watachukuliwa hatua.
Waziri jafo ametoa agizo Hilo mjini Dodoma wakati
akizindua ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji za makao makuu ya wilaya na
miji midogo nchini na kusema hakuna
sababu ya watu hao kuendelea kuwepo kama watakuwa wameshindwa kufikia asilimia
90 katika kufunga dira za maji.
Amesema baada ya kipindi hicho cha
miezi minne kupita na ikatokea kuna mamlaka ambayo haijafunga dira ya maji
atavunja bodi ya mamlaka hiyo na kumfukuza kazi meneja wake kwa kushindwa
kutimiza masharti hayo.
Amesema hatua hiyo imefikiwa ili
kudhibiti wizi wa maji ambao unafanywa na baadhi ya wateja kwa kushirikiana na
baadhi ya watendaji wa mamlaka za maji ambao siyo waamifu na hivyo kusababisha
mamlaka hizo za maji kujiendesha kwa hasara.
Kaimu
mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiri wa maji na nishati EWURA
NZINYANGWA NCHANY mamlaka za maji 56 Kati ya mamlaka 83 za wilaya na miji
midogo nchini hazina miundombinu ya kutibu maji kuua vimelea vya wadudu wa
magonjwa hali inayochangia kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko mara kwa Mara.
DK BINILITH MAHENGE ni mkuu wa mkoa wa Dodoma alipata nafasi ya
kuzungumza kama mwenyeji wa mkoa huo amesema mamlaka za maji zikizingatia
ufungaji wa dira za maji katika maeneo yao itasaidia kuweza kujiendesha kwani
zitaongeza mapato yao.
Ripoti hiyo ya EWURA imeonyesha kuwa hali ya
uzalishaji wa maji safi na salama katika mamlaka hizo ni 34.3 ya mahitaji
yanayohitajika katika mamlaka za makao makuu ya wilaya na miji midogo.
Mwisho.
Virus-free. www.avast.com |
Comments
Post a Comment