KIPINDUPINDU CHAUA 8 MPWAPWA .
JUMLA
ya watu 8 wameafiriki dunia
kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu na wengine 189 wamegundulika kuumwa ugonjwa huo katika wilaya ya Mpwapwa mkoa wa
Dodoma tangu ugonjwa huo ulipotiwe kuingia wilayani humo nov 2017 .
Mganga
mkuu wa wilaya hiyo Dkt Said Mawji aliyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa
katika kikao cha baraza la madiwani mjini Mpwapwakilicho fanyika hivi karibuni.
Mawji
alisema kuwa mgonjwa wa kwanza aligundulika octoba mwaka jana
akitokea kata ya Chipogoro na
wagonjwa wengine waliendelea kujitokeza kutoka katika kata mbalimbali hadi
kufikia wagonjwa 189 tangu ugonjwa huo
uanze hadi sasa.
Aliongeza
kuwa hadi kufikia feb mosi mwaka huu kulikuwa na wagonjwa wapya 14
ndio waliolio lazwa katika kambi
maluum ya kuwashughulikia wagonjwa
wa kipindupindu .
Aidha
alisema chanzo kikubwa cha ugonjwa huo
katika kata hizo ni kutokana na kuwapo kwa tatizo la uhaba wa maji na hivyo watu hulazimika kutumia maji ambayo
si safi na salama ambayo ni maji ya
visima vifupi ambavyo ni visima vya kienyeji ambavyo vimetuamisha maji ya mvua
na maji ya mtiririko katika kipindi hiki cha mvua.
“Katika
kata zenye ugonjwa wa kipindupindu tatizo kubwa la maji safi na salama kutokana na
hali ya uhaba wa maji watu
wanatumia maji amabayo si safi na
salama ambayo ni maji ya visima vifupi vya kienyeji(mikarama) na maji ya
mtiririko ambayo si salama sana”aliongea
aiongea Mawji.
Alisema
chanzo kingine kilicho changia kuenea
kwa ugonjwa huo kirahisi ni watu
wengi katika kata hizo kuto kufuata
kanuni za afya na kuto kuwa na vyoo hivyo hujisaidia vichakani pia mwingiliano wa
watu katika kata za mipakani kama kilosa na Chamwino na Kilolo na,kusababisha ugonjwa huo kulipuka kutokana na husaidia
kusambaza wadudu hao kirahisi na maji machafu kunchanganyika na maji ya visima.
Alisema kutokana
hali hiyo wamechukua hatua y ya
kutoa elimu ya kanuni za Afya ikiwamo kuchemsha Maji, yote ya visima kwa kuyawekea
dawa maluum ili kuweza kuua wadudu wote ambao wanaweza kusambaza ugonjwa huo kwa watu kirahisi na
kuwahamasisha watu kufuata kanuni za afya.
Mawji
alisema kwa sasa wananchi
wanapatiwa elimu ya kuhakikisha wanaishi
katika mazingira salama
ikiwa ni pamoja na kuwa
na vyoo bora kwa lengo la kujiepusha na mlipiko wa
magonjwa kama hayo na magonjwa
mengine ya mlipuko.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri alisema katika kata ambazo wagonjwa wametoka kwa
wingi wameuunda kamati za kudhibiti na kutoa elimu ya kanuni za afya na suala la usafi wa mazingira ili watu na jamii hiyo kuishi katika mazingira mabayo ni salama zaidi
ambazo kamati hizo zinaongozwa na madiwani wa kata.
Katika wilaya hii tayari kata zilizo kuwa na
wagonjwa wengi zilikuwa ni Iwondo,Mtera,Rudi,Masa Chipogolo na Mlunduzi
Kwa
sasa katika mkoa Dodoma wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya ambayo ugonjwa wa kipindupindu
umeumkumba kwa kasi ukiachilia mbali
wilaya ya kilosa Kongwa,Kilolo mkoani Iringa .
Mwisho.
Comments
Post a Comment