UCHUMI WA MADINI UTAKUZA UCHUMI WA VIWANDA NCHINI.
UCHUMI WA MADINI NA UTASAIDIA UCHUMI WA VIWANDA TANZANIA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe John Pombe Magufuli.
Tanzania ni nchi
iliyojaliwa na utajiri
mkubwa wa madini ya aina mbalimbali kama yenye thamani kubwa kama
,Dhahabu,Fedha,Chuma,zink,Shaba,Nikel,bati Urani na mengine mengi.
Wawekezaji
wamekuwa wakifutiwa na kubembelezwa kujakuwekeza nchini katika sekta ya madini ili
nchi iweze kuendelea ,uchumi wa madini ilianza kusikika kuanzia miaka ya themanini,kufuatia ongozeko
la ushiriki wa wawekezaji wa kigeni
katika sekta hii ya madini.
Tangu mwanzo ni kwamba madini yalitumika
kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji
viwandani hasa kwa mawe yenye madini.na sehemu muhimu ya
biashara ya ndani na kimataifa,madini
yenye manufaa kiuchumi ambayo si
metali ni grafati,baadhi feldisipa,kwatzi,almasi
na chembechembe nyingi ningene
zenye thamani kubwa kutokana na umuhimu
wake kimatumizi.
Kutokana na njinsi
zama za zinavyo pangwa ,zama
za mawe zama za shaba,nyeusi,bronze,zama
za chuma zama za dhahabuna kadhalika.
Mchakato wa mzima
wa uzalishaji una adhari kubwa kitaifa na kimataifa katika uhusiano wa
kijamii kisiasa na kiuchumi.
Ulimwenguni kote ili
viwanda viweze kuzalisha hutegemea takribani asilimia 80 ya madini na metali
mengi ya madini hayo ambayo hupatikana kwa wingi Afrika.
Mashirika ya kigeni
yalianza kuokodolea macho Tanzania mnamo
nusu ya pili ya miaka ya themanini,palebaadhi
ya mashirika hayo yaliyopopewa leseni za kutafuta na kuchimba madini,kabla ya
kupitishwa kwa sheria ya taifa ya uwekezaji (NIPP)ya mwaka 1990 kuanzishwa
kwa kwa kituo cha kuhamasiosha uwekezaji ( IPC) .
Sheria hii iliweza
kulegeza mashrti ya sera ya uchimbaji
madini ,sheria hii iliondoa kabisa ukiritimba
na udhibiti wa serikali katika msuala ya uchimbaji madini hata pale
serikali ilipokuwa na hisa.
Baada ya Rais awamu ya tano
Rais Dkt John Pombe Magufuli kuingia
madarakani alibaini madudu katika
idara hiyo kuwa pamoja na kuwapo kwa rasimali hii muhimu haikuweza kuisadia
Serikali katika kutatuaa changamoto za kiuchumi ambapo ilionekana
rasimali hiiilikuwa ikiwanufaisha
wawekezaji.
Kufuatia hali hiyo Rais alilazimika kuunda tume ya
kuchunguza udongo /chembechembe za
mchanga ambazo zimeamabatana na aina nyingi za madini tume iliyo julikana kwa tume ya makinikia iliongozwa na Pro Mruma .
Baada ya tume hiyo kuchunguza na ilitoa taarifa
yake tarehe 17.10.2017 iliweza kubaini ,ubadhilifu,uwizi na mikataba
isiyo rafiki kwa serikali inayo
pelekea madini mengi kutoroshwa nje na
kuiacha Tanzania ikiambulia mashimo na uharibifu mkubwa wa Mazingira .
Pro Mluma akisoma taarifa alisema kumekuwako utoroshwaji mkubwa wa madini
uliopelekea hasara ubwa
serikali na hivyo kupelekea baadhi ya watendaji wa wizara hiyo
kuiuzuru nyadhifa zao kutokana na
kushidwa kusimamia utendaji katika wizara hiyo ambayo ni miongoni mwa
wizara za msingi kiuchumi.
Baadhi ya wananchi wa
Mpwapwa wanampongeza Rais Joseph Pombe
Magufuli na kusema kuwa tangu aingie madarakani ameweza kusimamia rasmali za nchi ,utendaji serikali na
kupunguza ubadhilifu wa Fedha za umma.
Mwenyekiti wa
waachimbaji wadogo wa madini
mkoani Dodoma bwana Kulwa Mkalimoto alisema tangu Rais aingie madaraka kumekuwako na mabadiliko makubwa katika idara hiyo na fursa za wachimbaji wadogo kuanza
kuonekana ,kuwezeshwa mitaji,ujuzi ,na mikopo ili kuweza kusogezambele uchumi
wa nchi yetu.
Madini ya Zahabu yanavyo onekana.
Bwana Mkalimoto alidai kuwa
sambamba na wachimbaji
wadogo kuwezeshwa lakini pia kuna
mahusiano yamekuwa makubwa kati
serikali na wachimbaji hao ambayo
hapo awali haikuwa hiyo ambapo Mkalimoto anasema yamesabaishwa na utendaji
wa Rais wa awamu ya tano katika kusimamia
rasilmali za wanyonge nchini na
hivyo kusababisha kukua kwa
uchumi nchini.
Mmoja wa watalaamu
na mchambuzi wa masuala ya kiuchumi
na mwalimu wa chuo cha Mipango
mjini Dodoma ambae hakutaka jina lake kutajwa alisema baada ya mwaka
mmoja tu Rais Kuwa madarakani tuliweza
kuona ongezeko kubwa la fedha kwenye
miradi ya maendeleo kama
Afya,Maji ,Elimu ,barabara ,na miradi mingine mingi ,lakini pia alisema pia
ndani ya mwaka mmoja uchumi wa Tanzania uliweza kukua kwa kwa asilimia 7 wakati lengo likiwa kukua hadi
kufikia asilmia 7.9
Mchambuzi huyo
alisema “Rais amekaliliwa akisema Nchi hii ni tajiri na ni kweli ni tajiri nchi
hii ina ina aina nyingi za madini mengine ambayo hayapatikani
mahala pengine popote duniani lakini
Tanzania yapo na mengine yanazidi kugundulika ni lazima tumsaidie Rais
kusimamia utajiri tulio nao katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa
kati na Tanzania ya viwanda maana kupanga ni kuchagua”aliongea Mtaalamu
huyo.
Mchambuzi huyo alisema
ni lazima watanzania watambue Maslahi mapana
ya nchi na kuacha kulalamika juu
ya hali ya maisha bali wajibidishe katika kufanya kazi na kumsaidia
Rais kufikia Tanzania tunayo itamani ya uchumi wa kati.
Comments
Post a Comment