WANANCHI WA MPWAPWA WALILIA GARI LA ZIMA MOTO.
Moto
wateketeza nyumba na mali zenye
dhamani ya shilingi million 34 mali ya Bwana Mohamed Mounsor (Mokili)mkazi wa
kota Kata ya Mpwapwa mjini.
Bwana Monsour amesema kuwa chanzo cha moto
huo bado hakijajulikana ila serikali kwa
kushirikiana na shirika la Tanesco wanafanya uchunguzi wa kujua chanzo cha moto huo uliweza kuteketeza nyumba
yenye vyumba vitano, na bidhaa za ndani vyote
vyenye dhamani ya shilingi
million 34.
Kutokana na hali hiyo wananchi wa mji huo wameitaka uongozi wa
wilaya hiyo kuwa na gari la Zima moto
ili kuweza kukabiliana na majanga
ya moto.
Akiongea mwenyekiti wa mtaa wa kota Bwana Mwakiseyo ya katika
tukio la Nyumba ya bwana Mohamed Monsour (Mokili) baada ya kuungua moto na
kusidwa kuzima moto huo kutokana na wilaya hiyo kuto kuwa na gari la zima moto.
Bwana Mwakiseyo amesema pamoja na wilaya hiyo
kuwa ni miongoni mwa wilaya Kongwe hapa nchini na wilaya iliyo zungungukwa na tasisi nyingi za
serikali lakini imeshidwa kuwa na gari la zima moto kitu alichosema mala tukio
la moto likitokea mali huteketea zote.
Aidha amesema
kwa sasa wilaya hiyo imekuwa na matukio kadhaa ya nyumba za watu na
tasisi za serikali kuungua moto na mali nyingi za watu kuuteketea kabisa .
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama ambae ni mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri alisema kuwa
katika tukio hilo hakuna mtu
aliye weza kupoteza maisha bali aliamuru
jeshi la polisi kwa kushirikiana na shirika la ugavi wa umeme TANESCO kufanya uchunguzi wa haraka wa
kubaini chanzo cha moto huo.
Shekimweri amesema kutokana na wilaya hiyo
kuwa na matukio kadhaa sasa ya moto na ukuaji wa mji huo na Mpango wa serikali kuhamia mkoani Dodoma kuna haja ya wilaya hiyo kuwa kuwa na gari la zima moto na kikosi cha zima
moto katika wilaya hiyo ili kuweza kunusuru mali za wananchi au za serikali
kuteketea .
Comments
Post a Comment