WANAFUNZI WA AWALI IDILO MPWAPWA WASOMEA CHINI YA MITI.
WANAFUNZI WA awali katika shule ya msingi
Idilo wilayani Mpwapwa mkoani
Dodoma huwalazimu kusomea chini ya miti kutokana na uhaba wa vumba vya madarasa sheleni hapo.
Wanafunzi hao waliokutwa na majira wakiwa wamekaa
kwenye viti vya matofali huku
wakiwa chini miti na darasa linaendelea.
Ofisa elimu kata ya Mazae Bwana Betweli
Sanga alikili wanafunzi hao kusomea chini ya miti
kitu alicho sema kinasababishwa na uhaba
wa wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Sanga alisema kwa sasa shule hiyo inavyumba vya madarasa 7 wakati mahitaji ni vyumba 10 na kupelekea kuwa upungufu wa vyumba vitatu
vya madarasa shuleni hapo.
Sanga alisema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi
290 wakiwamo wavulana 129 na wasichana 120lakini inavyumba saba vya madarasa.
Aidha Sanga alisema pamoja na uhaba wa vumba
vya walimu pia shule hiyo inakabiliwa na chanagamoto ya nyumba za
walimu,matundu ya vyoo,pamoja na vifaa vya kufundishia
Kufuatia hali hiyo uongozi wa kijiji
hicho umeamua kijenga chumba kimoja cha wanafunzi hao ii kuweza kuwandoa wanafunzi hao kusomea
kwenye miti kukaa chini na kuwataka wasomee kwenye darasa la kisasa lenye hadhi
ya kusomea wanafunzi wa awali ambalo
litakuwa na ofisi yake pamoja choo
chake ili kuyaboresha mazingira ya watoto hao kupenda shule.
Kwa mujibu
wa mwenyekiti kijiji cha Idilo bwana Grasion Mkokoten alisema wameamua kufanya hivyo
kutokana ni wajibu wao kama serikali ya kijiji pamoja na wananchi wa
kijiji hicho kuweza kushiriki katika
maendeleo yoyote katika kijiji chao ili
serikali iweze kuwaunga mkono katika umaliziaji.
Bwana mkokoteni alisema kutokana na wanafunzi hao kusomea chini ya miti
kumepelekea wanafunzi wengi wa awali kutopenda shule ,hivyo kusababisha wazazi
wengi kuto kuandikisha wanafunzi hao
walio fikia umri wa kuanza darasa la awali kuto andikishwa.
Comments
Post a Comment