DC atangaza vita na waharibifu wa mazingira mpwapwa.
Mkuu
wa wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri ametangaza vita na
watumishi wa serikali watakao bainika katika
kuihijumu serikali katika vita ya
kupambana na uharibifu wa mazingira
Mpwapwa.
Shekimweri aliyasema hayo ofisi kwake alipo
kuwa akiongea na waandishi juu
mikakati ya kuikomboa wilaya hiyo juu ya uharibifu wamazingira.
Mkuu wa wilaya hiyo alisema kupitia kamati ya ulinzi na usalama
imebaini baadhi ya watumishi wa serikali wamekwa wakihusika katika uharibifu wa
mazingira kwa kuwa na vibali feki ya
kuchana mbao .
Aidha alisema
watumishi wote waliotuhumiwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za
kinidhamu na hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakama kujibu tuhuma zinazo wakabili.
“Inasikitisha
kuona watumishi wenzangu wa serikali
kujikita katika sula la uharibifu
wa mazingira ,kwa hili sitakuwa na uvumilivu hata kidogo katika mazingira mimi
nina zero tolelance lazima wote wachukuliwe hatua na wafikishe
mahakamani.”aliongea
Kwa mujibu
wa mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir
Shakimweri alisema kuwa tadhimini iliyo fanywa na Baraza la mazingira Tanzania NEMC limebaini kuna baadhi ya madahara yanayo tishia uendelevu wa wilaya hiyo kiuchumi na kijamii.
Shekimweri
alisema kwa sasa kuna uharibufu mkubwa wa
mazingira katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Mpwapwa kitu alicho sema kuwa kinatokana na
baadhi ya ya viongozi kushidwa kusimamimia
sheria ,uzembe ,kuzoeana na mianya ya rushwa kuanzia kamati za
mazingira ngazi za vijiji na kata.
Aidha
Shekimweri kufuatia hali na hiyo imeonyesha kuwa Mpwapwa siku si nyingi
inaweza kugeuka jagwa kutokana na wananchi kulima katika vyanzo vya maji, kuchoma mazingira,na
kulima katika misitu ya uhifadhi pamoja na kukata miti ya asili iliyo kuwa
chanzo kikuu cha kuvuta maji katika ardhi.
Pia alisema kufutatia taarifa hiyo
kumenyanyua kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuweza
kuweka mikakati kabambe ya
kuirudisha Mpwapwa katika uoto wake wa asili kama ilivyo kuwa asili kwa kuweka
uhamasishaji,kuweka mikakati ya usimamizi wa sheria kwa kujengea uwezo mabaraza la kata pamoja na
kamati za mazingira ngazi za vijiji hadi kata.
“Kwa kweli
mimi kama mkuu wa wilaya sitakiwi kulalamika
ninachotakiwa kukifanya ni kutoa majibu katika hiki kisicho kuwa na majibu
hasa katika mazingira ,kwa kweli sina uvumilifu hata kidogo tumeweka
mikakati kababmbe ya kuirudisha mpwapwa katika uoto wake wa asili kama ilikuwa awali”aliongea Shekimweri.
Alisema matokeo ya uharibifu wa mazingira ni
mkubwa ambapo katika vyanzo vya maji vya
mtililiko katika mji wa Mpwapwa vilivyo
kuwapo ni chanzo kimoja tu ambacho kimebaki cha Mayawile nacho kikendelea
kukauka kila kukicha .
Alisema kuwa
Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya ambazo haziko vizuri katika utanzaji wa
mazingira na misitu ya asili kwa watu kuchoma ,kulima na kukata miti katika vyanzo vya maji na
katika vilele vya milima .
Aliongeza
kuwa tayari wilaya ya Mpwapwa
imeshanza kukubwa na matokea ya tabia ya nchi kwa kuongezeka kwa joto,
kupungua kwa mvua na kukauka kwa baadhi ya vyanzo vya maji ambayo vilikuwa ni
tegemeo kubwa kwa maisha ya wakazi wa mpwapwa na viunga vyake kwa kuendesha
maisha ya kila siku.
Comments
Post a Comment