HAKI ELIMU WATAMBULISHA MKAKATI WA MIAKA MITANO MPWAPWA.
SHIRIKA lisilo
kuwa la kiserikali linalojihusisha na ushawishi katika kuboresha Mazingira ya
Elimu hapa nchini la Haki Elimu limeiomba
serikali kuendelea kushughulikia chamngamoto zinazo ikabili Elimu kwa sasa ili
kuweza kuwa wataalamu wenye tija siku za
mbeleni.
Kauli hiyo ilitolewa na wadau wa elimuwilayani hapa katika kikao cha pamoja na shirika la Haki Elimu walipokuwa wakitambulisha mkakati wao wa miaka
mitano utakao fanywa na shirika hilo juu ya kuweza kuinua
Elimu hapa nchini.
Ofisa Programu wa
shirika hilo bwana Frolige Lyelu amesema pamoja na serikali kuonyesha nia dhabiti ya kuikomboa elimu hapa nchini lakini kuna bado baadhi ya
changamoto ambazo zinatakiwa kumalizwa na ngazi za chini kuliko kuendelea kuisubiri serikali .
Frolige alisema Mpango
wa Elimu bila malipo umeweza kuongeza hamasa ya watoto wengi kuandikishwa darasa la kwanza na wanao jiunga kidato cha
kwanza idadi imekuwa ikiongezeka kila mwaka kitu alichosema kuwa kinaonyesha kuwa michango mingi shuleni ilikuwa ni chanzo
watoto wengi kukosa Elimu.
Hata hivyo amesema
bado kuna uelewa mdogo wa jamii kuhusu mapango wa Elimu bila malipo na ushiriki wao katika katika shughuli
za maendeleo ya Elimu.
Pia Frilie amesema kuwa pia serikali inatakiwa kushughulikia changamoto ya farsafa ya elimu kwa sasa
kutokana na elimu yetu kutokuwa na farsafa “tunakumbuka wote katika serikali ya
awamu ya kwanza tulikuwa na farsafa ya elimu na kujiteemea lakini hivi sasa
farsafa ya elimu ni ipi hivyo kutokuwapo
na farsafa kunapelekea kushidwa kuwa na mwelekeo wa elimu”aliongea.
Hata hivyo Ofisa
Progamu huyo alisema katika miaka mitano shirika la haki Elimu
nakusudia ,kushawishimabadiliko ya kisera
na utekelezaji wake,kukuza ushiriki wa wananchi na kujishughulisha,na
kukuza uwazi na uwajibikaji katika maeneo ya serikai za vijiji na shule.
Kwa upande wake kaimu Ofisa Elimu Elexender Kioyi alikili kuwapo kwa changamoto nyingi katika
idara ya elimu kwa wilaya yake ikiwemo vyumba vya madarasa,upunufu wa vifaa vya
kujifunzia na kufundishia,pamoja na vyumba vya awali na matundu ya vyoo kwa
wanafunzi wenye umri mdogo ambapo baadhi
ya shule wanafunzi wa awali husomea nje kwenye miti sana kitu alicho kisema pia
nacho ni sababu inayo changia elimu kurudi nyuma.
Kioyi alisema kama wadau wa maendeleo wakashirikiana na serikali tunaweza kuikomboa
serikali na kufika tunapopatarajia .
“Mwanafarsa mmoja aliwahi kusema kuwasehemu ya mabadiliko
unayotaka yatokee dunia kuliko kubaki kupiga kelee tu,kwa mpango haki elimu
naona wao pia wameona baada ya kufanya utafaiti wameingia nao kuwa sehemu ya
mabadiliko”aliongea Kioyi.
Comments
Post a Comment