DC agundua chang za maji mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akikagua baadhi ya mitambo ya maji katika kisima cha Kiombo.
ZAIDI
ya wakazi 29,422 wa mji wa mpwapwa na viunga
vyake hutumia maji machafu yasiyo tishia
kutokea kwa magonjwa ya mlipuko
yanayosababishwa na matumizi maji maji machafu.
Hali
hiyo imebainishwa na Mkuu wa wilaya ya
Mpwapwa mkoani Dodoma bwana Jabir Shekimweri baada ya kutembelea vyanzo vya maji vinavyo
saidia kusambaza maji katika mji wa Mpwapwa.
Pia
Shekimweri abaini changamoto lukuki
zinazosababisha Mji wa Mpwapwa kuto kuwa na maji ya uhakika japo ya kuwa na
mradi mkubwa wa maji ulioghalimu jumla
ya shilingi billion4.
Aidha
changamoto zilibainishwa na mkuu wa wilaya hiyo ni maji yanayotumiwa na wakazi
mpwapwa ni machafua ambapo tumbili,Ngedele na wanyama wa poli kuyatumia na kuoga
humo kutoka na chanzo hicho
kutokuwa na uzio wa kuweza kuzuia wanyama kuchafua kwenye
vyanzo hivyo.
Pia
ufanisi hafifu wa mradi wa maji chumvi
ujulikanao kama mradi wa mkenya iliogharimu jumla ya shilingi billion 4/=
uliofadhiliwana serikali ya Kifaransa uliojegwa na kampuni ya Oliento kutoka
nchini Kenya ambao ulitegemewa kuwa mkombozi wa adha ya maji katika mji wa
Mpwapwa, ambapo hali hiyo imekuwa tofauti
kwa mradi huo ambao kwa sasa wakazi wa mji wa mpwapwa hupata maji kwa
zamu kwa siku moja hadi mbili kitu kinachowatia wasiwasi wakazi wa mpwapwa kuwa labda mradi huo na
vifaa vilivyo wekwa haviendani na thamani
ya fedha.
Kufuatia
hali hiyo mkuu wa wilaya ya Mpwapwa ametoa
siku 30 kwa mamlaka ya maji mjini hapa MPWAUSA kuweza kufanya malekesho yote kwenye vyanzo
vya maji ikiwemo kuyafanyia usafi matanki yote
yanayosaidia kusambaza maji katika mji wa mpwapwa, ili kuweza kujikinga na magonjwa ya mlipuko
na magonjwa mengine yanayo sababishwa na kutumia maji machafu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
mamlaka wa maji safi na Mazingira MPWAUSA Bwana Peter Kabelwa amekili mradi huo kutoa huduma chini ya
kiwango, ambapo alisema kwa maelekezo ya mradi yalitakiwa mashine
zizalishe maji ujazo wa lita 80,000kwa
saa lakini kwa sasa mashine hizo huzalisha lita 45,000 kwa sasa tofauti na
maelekezo ya mradi.
Kutokana
na hali hiyo uongozi wa mamlaka ya tumejipanga kufanya uchunguzi wa uwezo wa
mashine zilizo wekwa kwa ajili ya usambazaji wa maji mjini hapa kitaalamu
tunaita (Pumpu tsting)aliongea
Comments
Post a Comment