WAIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI WAASWA KUFUATA MAADILI.
. WAIMBAJI wa nyimbo za dini Nchini wamekumbushwa kutunga nyimbo za kuhamasisha Amani na watu kupenda kufanya kazi. Sambamba na hilo pia waimbaji wa kike wa Music wa dini wametakiwa wasimame katika uwakili wa kazi ya Mungu ya kuomba kwa ajili ya Taifa na kuombea familia na kubaki katika maadili ya music wao unavyo wataka . Rai hiyo imetolewa jana wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma na Meneja wa Bank ya NMB tawi la Mpwapwa Bi Beatrice Mwasa katika Uzinduzi wa Album ya mwimbaji wa nyimbo za Dini Mwalimu Paulina Ndatila(Mwl Boma) albam inayojulikana kwa jina la TUTATAWALA. Bi Mwasa alisema kumekuwako na upotovu wa maadili kwa baadhi ya waimbaji wa nyimbo za dini kwa uvaaji wao ambao hauakisi kile wanacho kiimba Pia alisema waimbaji hao wakitunga nyimbo za njisi ya kupunguza migogoro ya familia ambayo inatishia kuongezeka ...