Posts

WANANCHI WALALAMIKIA HUDUMA HAFIFU TANESCO MPWAPWA.

Image
WANANCHI wa wilaya ya Mpwapwa   mkoani Dodoma   wamelalamikia huduma duni na hafifu za shirika la   ugavi la umeme TANESCO   wilayani hapa kuwa zinawarudisha nyuma kimaendeleo Wananchi hao waliyoataoa malalamiko yao walipo kuwa wakiongea na mwandishi wa habari   juu ya kuto ridhishwa na huduma zitolewazo na shirika hilo kuwa   zimekuwa za   kusuasua na huchukua muda mrefu kushughulikiwa kero zao kitu   walicho kisema kuwa   kinachangia kudumaza uchumi na maendeleo ya watu wa Mpwapwa. Mmoja   wa wananchi   wa wilaya hiyo bwana AHMAD UTAMU   alisema kumekuwa na ubabaishaji wa   ujazaji wa ramani pindi unaomba     huduma za kuunganishiwa   umeme ndani ya nyumba,kukatika katika kwa umeme mara kwa mara   kunakopelekea baadhi ya watu kuunguza vitu vyao na kuwasababishia hasara kubwa. Aidha bwana Ahmad   alisema kuwa   shirika hilo limekuwa likikiuka mkataba wa huduma kwa mteja ...

KOROSHO MKOMBOZI WA UCHUMI KWA WAKULIMA MPWAPWA

Image
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabiri Shekimweri akikagua kitalu cha Miche ya Korosho. SERIKALI Wilayani   Mpwapwa   mkoani Dodoma yawapa changamoto   wanaufaika wa   wa Mpango wa kaya maskini   TASAF   kuacha kutegemea fedha za ruzuku yawataka kujikita katika   kilimo cha Korosho   ili kuwa na uchumi endelevu. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri     juzi alipotembelea miradi uoteshwaji wa miti na vitalu vya korosho   ya   wanufaika   wa Mpango wa   katika vijiji vya   Idilo,Gulwe,Kingiti na Iyenge. Shekimweri alisema   wao kama serikali lazima wawasaidie wanafaika wa mpango huo kuweza kuwa na   uchumi endelevu kwa kujikita katika ulimaji wa zao la korosho ambalo ndani ya miaka mitatu linaweza kubadilisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na kaya kwa ujumla kuliko kutegemea   fedha hizo za   ruzuku   ya kila mwezi ambazo zitamsaidia   kupung...

NCHEMBA ALAANI VITENDO VYA KIHARIFU.

Image
  WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amelaani vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa vikitokea katika maene mbalimbali nchini ikiwemo mauaji,vitendo vya utekaji,kupigwa na kutishiwa risasi kwa baadhi ya viongozi,wananchi pamoja na wanasiasa vilivyofanywa katika kipindi cha mwaka 2017. Kutokana na hayo Waziri Mwigulu ameitaka jamii katika mwaka 2018 kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya kiuhalifu. Hata hivyo Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi inakutana na waandishi ili kueleza mipango mikakati ya kutokomeza vitendo vya uhalifu mwaka huu Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi mjini Dodoma,Waziri wa wizara hiyo Mwigulu Nchemba amesema kuwa ili kutokomeza vitendo vya kiuhalifu jamii inatakiwa kuwa mustari wa katika kutoa taarifa za wahalifu. Waziri Mwigulu akazungumzia namna wizara kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ilivyojipanga kwa kipindi cha...

MAJI KIKWAZO CHA MAENDELEO IDILO WILAYA YA MPWAPWA

New post el-Mpwapwa Wakazi  wa kijiji cha Idilo kata ya Mazae wilayani  Mpwapwa mkoani hutumia maji yasiyo salama  na kutishia kupata magonjwa ya mlipuko hasa kipindi hiki kuelekea msimu huu wa mvua za vuli. Maji hayo yanayopatika  umbali km 2 hadi 3 kwa  pia ni maji ya makorongoni ambayo  ni hatari kwa afya za wakazi hao. Diwani wa kata hiyo  bwana Wiliam Vahae   amesema  wakazi hao hulazimika kuamka alfajili na mapema ili kuwahi maji katika kisima kabla hayajachafuliwa na wanyama  wa polini lakini kabla ya wafugaji hawajanza kunywesha  Ng,ombe ambao wanakuwa na makundi makubwa ya mifugo. Aidha Vahae amesema kutokana na hali hiyo  kumepelekea wakazi wa kijiji hicho kutumia maji ya visima vya asili na makorongo ambayo si safi na salama na kutishia magonjwa ya mlipuko kama kipindupindi. Amesema kufutia tatizo hilo tayari wakazi wa kijiji hicho wamesha changa kiasi cha shilingi million 450,000/=ambazo ...

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU UWT WAAONYWA DODOMA.

WAJUMBE wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa  Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Dodoma wameaswa kuchagua viongozi makini na imara watakaokifanya chama kiendelee kuwa imara kutokana na  mkoa huo kuwa makao makuu ya Chama. Pia amewataka wana CCM kupendana,kupunguza figisu,visasi,majungu,porojo na kuwa ili kufikia maengo ni lazima wanyanyuane na kuinuana kwa lngo la kumfanya kila mmoja atimize yale aliyoyapanga kwa msaada mkubwa wa mwanamke. Rai hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Dodoma Alhaj Kimbisa wakati akifungua mkutano huo ambapo amesema CCM nyumbani kwake ni Dodoma hivyo viongozi watakaochaguliwa lazima watambue hilo kwa kulinda heshima isipotee. Aidha amewaasa kutochagua viongozi wenye harufu ya rushwa bali wachague viongozi watakaokuwa wepesi wa kuwaunganisha akina na watakaoifanya jumuiya ijitegemee kiuchumi. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe 473  ambapo miongoni mwa nafasi zinazogombewa ni nafasi y...

WAZIRI ATAKA CHANGAMOTO ZA MAJI KUISHA VIJIJINI

Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi Izack Kamwelwe amesema katika kukabiliana na kero ya upatikanaji wa huduma ya maji wilayani Kongwa mkoani Dodoma serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya miradi ya maji wilayamo hiyo. Wilaya ya Kongwa ni miongoni mwa wilaya kongwe zilizopo makao makuu ya nchi Dodoma licha ya ukongwe wa wilaya hiyo bado wananchi wake wanateseka kutafuta huduma ya maji na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu. Hali hiyo inamlazimu Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Izack Kamwelwe anafanya ziara wilayani humo na kutoa matumaini mapya kwa wananchi katika kutatua tatizo hilo sugu na kuahidi serikali itamaliza tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo ndani ya muda mfupi. Mhandisi Izack Kamwelwe Waziri wa maji na umwagiliaji Deo Ndejembi ni mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara amesema kuwa atahakikisha anasimamia ujenzi wa miradi ya maji ili wananchi waweze k...

KOROSHO ITAGEUZA UCHUMI WA DODOMA

WAKULIMA  wa Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kujikita katika ulimaji wa zao la korosho kwani zao hilo lina faida kubwa kibiashara tofauti na yalivyo mazao mengine.  Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara nchini. Kwa sasa zao hili hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania, yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga. Takwimu kutoka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) zinathibitisha umuhimu wa zao hilo kwa Taifa, ambapo katika msimu wa 2012/13 zao hilo liliiingizia Serikali kiasi cha Sh bilioni 29.5 kutokana na ushuru wa usafirishaji wa korosho ghafi nje ya nchi. Akizungumza wakati wa ziara yake katika baadhi ya wilaya za mkoa huo  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.Binilith Mahenge ameeleza kuwa utafiti umefanywa na kubaini ardhi ya Dodoma inafaa kwa uzalishaji wa zao hilo. Akitoa taarifa ya wilaya kwa Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota amesema wilaya yake imeanza kuwa na mkakati wa zao la korosho kama zao la biashara n...