Posts

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU UWT WAAONYWA DODOMA.

WAJUMBE wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa  Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Dodoma wameaswa kuchagua viongozi makini na imara watakaokifanya chama kiendelee kuwa imara kutokana na  mkoa huo kuwa makao makuu ya Chama. Pia amewataka wana CCM kupendana,kupunguza figisu,visasi,majungu,porojo na kuwa ili kufikia maengo ni lazima wanyanyuane na kuinuana kwa lngo la kumfanya kila mmoja atimize yale aliyoyapanga kwa msaada mkubwa wa mwanamke. Rai hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Dodoma Alhaj Kimbisa wakati akifungua mkutano huo ambapo amesema CCM nyumbani kwake ni Dodoma hivyo viongozi watakaochaguliwa lazima watambue hilo kwa kulinda heshima isipotee. Aidha amewaasa kutochagua viongozi wenye harufu ya rushwa bali wachague viongozi watakaokuwa wepesi wa kuwaunganisha akina na watakaoifanya jumuiya ijitegemee kiuchumi. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe 473  ambapo miongoni mwa nafasi zinazogombewa ni nafasi y...

WAZIRI ATAKA CHANGAMOTO ZA MAJI KUISHA VIJIJINI

Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi Izack Kamwelwe amesema katika kukabiliana na kero ya upatikanaji wa huduma ya maji wilayani Kongwa mkoani Dodoma serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya miradi ya maji wilayamo hiyo. Wilaya ya Kongwa ni miongoni mwa wilaya kongwe zilizopo makao makuu ya nchi Dodoma licha ya ukongwe wa wilaya hiyo bado wananchi wake wanateseka kutafuta huduma ya maji na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu. Hali hiyo inamlazimu Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Izack Kamwelwe anafanya ziara wilayani humo na kutoa matumaini mapya kwa wananchi katika kutatua tatizo hilo sugu na kuahidi serikali itamaliza tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo ndani ya muda mfupi. Mhandisi Izack Kamwelwe Waziri wa maji na umwagiliaji Deo Ndejembi ni mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara amesema kuwa atahakikisha anasimamia ujenzi wa miradi ya maji ili wananchi waweze k...

KOROSHO ITAGEUZA UCHUMI WA DODOMA

WAKULIMA  wa Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kujikita katika ulimaji wa zao la korosho kwani zao hilo lina faida kubwa kibiashara tofauti na yalivyo mazao mengine.  Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara nchini. Kwa sasa zao hili hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania, yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga. Takwimu kutoka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) zinathibitisha umuhimu wa zao hilo kwa Taifa, ambapo katika msimu wa 2012/13 zao hilo liliiingizia Serikali kiasi cha Sh bilioni 29.5 kutokana na ushuru wa usafirishaji wa korosho ghafi nje ya nchi. Akizungumza wakati wa ziara yake katika baadhi ya wilaya za mkoa huo  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.Binilith Mahenge ameeleza kuwa utafiti umefanywa na kubaini ardhi ya Dodoma inafaa kwa uzalishaji wa zao hilo. Akitoa taarifa ya wilaya kwa Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota amesema wilaya yake imeanza kuwa na mkakati wa zao la korosho kama zao la biashara n...

WALIMU WAOMBA KUBORESHEWA MAZINGIRA MPWAPWA

MKUU wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bwana Jabil Shekimweri amewataka waajili kuto kuzalisha madeni Malta kwa wafanya kazi wakati serikali ipo kwenye mkakati mkubwa wa kulipa madeni kwa walimu. Mkuu wa wilaya huyo aliyasema hayo juzi alipo kuwa akifungua mkutano mkuu wa chama cha walimu wilayani hapo kwa mwaka 2017. Shakimweri alisema kuwa Tanzania ikiwa inajiandaa kuingia katika uchumi wa viwanda lazima kuwekeza katika Elimu ili kuweza kupata wataalamu watakao hudumu katika viwanda hivyo kwa mstakabali Tanzania mpya. "Tunapo zungumzia Tanzania ya Viwanda lazima tuwaze juu ya wahudumu katika viwanda hivyo lazima tuwajibike kutoa wanafunzi walio makini watakao fiti katika utaalamu wa viwanda" aliongea Shakimweri. Aidha Shakimweri ameendelea kuvipigia kelele vitendo vya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya walimu wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi, V walimu kumamatwa na vitendo vya rushwa na uwizi. Pia Mkuu wa wilaya huyo aliwata walimu hao kujihus...

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU TAHADHARI ZA MVUA.

SERIKALI imetoa tahadhari ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini huku ikielekeza wananchi kutumia fursa chanya za mvua hizo kwa shughuli za maendeleo kama kilimo kwa ajili ya kupanda mazao yanayohitaji maji. Mbali na kilimo pia wananchi wametakiwa kutumia mvua hizo kuandaa mabwawa na malambo kwa ajili ya uvunaji wa maji .    Tahadhari hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge, kazi, ajira,vijana na watu wenye ulemavu Stella Alex wakati akizungumza na waandishi wa habari. Amesema kuwa kamati za usimamizi wa maafa kuanzia ngazi ya kijiji na mtaa zinatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa maafa NO.7 ya mwaka 2015 na kanuni za usimamizi wa maafa za mwaka 2017. Amesema kuwa septemba 4 mwaka huu Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ilitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Octoba mpaka disemba mwaka huu kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua na...

UKATILI WA KINJISIA UWEKEWE MKAKATI MADHUBUTI

SERIKALI ya Mkoa wa Dodoma imewataka wakurugenzi wa wilaya zote ndani ya mkoa ,sekretarieti ya mkoa pamoja na watendaji wengine katika ngazi zote kutekeleza kwa vitendo majukumu yote waliyopangiwa kwa mujibu wa mpango wa kitaifa wa kutokomeza  ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Maagizo hayo yametolewa hii leo na kaimu mkuuwa mkoa wa dodoma ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga wakati wa ufunzguzi wa maadimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili dhidi ya wananwake na watoto ambapo mbali na hayo pia ametoa magizo kwa maafisa maendeleo na ustawi wa jamii huku akisistiza kuwa maagizo hayo yatafatiliwa kwa kadri itakavyotakiwa. Aidha pia Nyamoga amesema wananchi wengi wamekuwa wakiwatoa malalamiko  watendaji wa vijiji na kata kujihusiha na vitendo vya rushwa jambo ambalo linadidimiza jitihada za kutokomeza ukatili dhidi ya wananwake na watoto jambo ambalo kwa mkoa wa dodoma halikubaliki. Kwa upande wake mwakilishi wa katibu mkuu  wiz...

AHUKUMIWA MIAKA 60 JELA KWA KUBAKA WATOTO WA MIAKA 9 NA 12

MAHAKAMA ya hakimu makazi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imemuhukumu kifongo cha miaka 60 jela na kupigwa viboko kumi na mbili Bwana Aloyce Hela (45)  mkaz wa Mwanakianga baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji. Kesi hiyo iliyo kuwa inasikilizwa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bwana Pascal Mayumba ambapo ilivuta hisia za wakazi wa Mpwapwa na watetezi wa haki za watoto wilayani hapa. Bwana Mayumba ameiiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo katika tarehe Tofauti kuanzia mwaka 2015 hadi Sasa ambapo alikuwa akiwabaka watoto wawili wa miaka (9)na miaka (12) wanafunzi wa Darasa la pili na la kwanza katika moja wapo wa shule wilayani hapa. Mayumba amesema mtuhumiwa alifanya kosa kinyume na kifungu cha sheria 130na 131 kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu iliyo fanyiwa malejeo mwaka 2002. Aidha Mayumba ameambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa alifanya kosa hilo zaidi ya mala mbili na kuwapa watoto hao shilling 200 na alikuwa anafanya katika ...