Bilioni 300 za vigogo Uswisi zatikisa nchi Send to a friend Tuesday, 26 June 2012 21:38 0 digg ZITTO AMTAKA PINDA ATAJE WAHUSIKA, WANANCHI WATAKA FEDHA ZIREJESHWE, MABILIONI ZAIDI YAIBWA MTANDAONI KUBAINIKA kwa Sh303.7 bilioni zilizofichwa katika akaunti za vigogo wa Serikali na wanasiasa nchini Uswisi, kumetikisa nchi huku shinikizo likitolewa kwa vyombo vya dola kuchunguza haraka na kuchukua hatua za kisheria, ikiwamo kurejesha fedha hizo. Jana kutwa nzima, gazeti hili lilipokea simu kadhaa kutoka kwa wasomaji wake wakiwamo wabunge na mawaziri, huku baadhi wakichangia maoni kwenye tovuti na mtandao mbalimbali ya kijamii, wakitaka kujua majina ya wamiliki wa akaunti hizo. Bungeni mjini Dodoma, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliitaka Serikali kuchunguza tuhuma hizo kisha kuwachukulia hatua watu sita wanaotajwa kwamba wanamiliki akaunti zenye mabilioni hayo ya shilingi chini Uswisi. Fedha hizo zimebainishwa...