WANANCHI WAMKATA MAPANGA MTUMISHI WA HALMASHAURI,KISA KIPINDUPINDU.
Jeshi la polisi
wilaya Mpwapwa Mkoani Dodoma linawashilikia watu wanne wa kitongoji cha Isalaza kijiji cha Igoji
II kwa tuhuma za kumjeruhi mtumishi wa Idara ya afya halmashauri ya wilaya bwana Yusuph Ridhiwani ofisa afya akiwa kazini .
Tukio hilo lilitokea march 03 mwaka huu katika kitongoji
cha Isalaza kijiji cha Igoji ii wilaya ya Mpwapwa na mkoa Dodoma baada ya
maofisa afya wa halmasahauri ya
wilaya ya Mpwapwa kwenda kwenye oparasheni ya kudhibiti kipindupindu.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Dodoma bwana Giles Mroto amethibisha kutokea kwa kutukio hilo na amesema chanzo cha mtumishi huyo kujeruhiwa na siraha za jadi
ilikuwa ni waananchi kuto taka
kusumbuliwa katika oparesheni ya kuzuia kipindupindi ambapo kwa Mpwapwa ugonjwa huo umedumu kwa
zaidi ya miezi mitano sasa tangu uingie mwezi nov mwaka jana.
Akiwataja watu
wanaoshikiliwa na jeshi alisema ni mwenyekiti
wa Igoji II bwana Gelezi Mlowela,Bahati Mwinyi holo,Eda Cholingo na Elei
Udoba.
Kamanda Mroto alisema
kuwa watumishi hao zaidi
10 walioenda kufanya kazi hiyo
kijijini hapo kudhibiti ugonjwa wa kipindu pindu kwa kuwakamata watu wasio na
vyoo na kuwatoza faini ndipo wananchi wakajikusanya na kuwashambulia watumishi
hao “walikuwa wengi zaidi ya sita wengine
walikimbia ndipo wakabahatika
kumkamata huyo mmoja na kuanza kupiga sehemu mbalimbali za mwili wake na
kumkata na vitu vyenye ncha kali”
Kamanda Mroto alisema
tayari watuhumiwa wamefikishwa
makahamani na kwa sasa wako maabusu katika gereza la Mpwapwa.
Akisimulia Tukio hilo
shuhuda tukio hilo na ofisa afya wa halmasahauri ya Mpwapwa bi Mery Mabagwa
alisema walipofika katika kijiji hicho
waligawana miitaa ya kufanya kazi ndipo
walipoanza anza kazi walipokuwa
wakiendelea na kazi walisikia kengele inagongwa na ndipo na ndipo wananchi walipo anza kuwavamia na
kuvamia gari ya polisi na kuanza kulipiga mawe ndipo dereva akaondoa gari na
kukimbia nalo kuanza kuwakimbiza
nakumkamata mmoja wao na kuanza kupiga na siraha za jadi.
Mabagwa alisema “baada
ya kumpiga na kumjeruhi mwezao kwa
siraha za jadi walidhani wamemua na
kumuacha akivuja damu pale chini wakati
huo polisi wote wamekimbia vichakani kujificha” alieleza ofisa
huyo
Mganga mkuu wa hospitali ya Benjamini Mkapa wilaya hapa
Dkt Said Mawji amekili mtumishi
wake kujeruhiwa akiwa kazini na alisema
walimjeruhi sehemu za kichwani,mkanoni
na kupiga na fimbo sehemu
mbalimbali za mwili wake kwa fimbo na malungu.
Dkt Mawji alisema kwa sasa mgonjwa huyo amelezwa kwenye wadi ya
namba 4 katika hospitali ya Benjamini Mkapa kwa matibabu na alisema “hali yake inakwenda
inabadilika badilika hivyo bado
haijatengamaa vizuri kutokana na kupata majeraha kichwani
lakini kwa sasa anaendelea na matibabu
na tunafanya kila linalowezekana
ili kuweza hali yake iweze kutengemaa.”alieleza
Comments
Post a Comment