BABA AMBAKA MWANAE WA MIAKA 12 NA KUMMPA MIMBA.
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Jemsi Leuna
mkazi wa kijiji cha Chitemo wilaya ya
Mpwapwa Mkoa wa Dodoma amefikishwa
mbele ya hakimu makazi mfawidhi bi
Nurupedesia Nassar kufutia tuhuma ya kumbaka na kummpa mimba mtoto wake wa
kumzaa mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa nne.
Mwendesha
mashitaka wa polisi Bwana Michael Joseph
aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo akitambua kuwa huyo ni mtoto wake wa kumzaa aliweza
kumbaka na kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha namba 130 kifungu kidogo(1) na
kifungu 131kifungu kidogo(1)iliyo fanyiwa malejeo mwaka 2002.
Bwana
Machael aliiambia mahakama kuwa kosa la pili ni kummpa mimba mwanafunzi darasa la nne
kinyume na sheria ya Elimu namba 353
kifunfu cha 60Akifungu kidogo cha kwanza
iliyofanyiwa malejeo mwaka 2016.
Mtuhumiwa
alipo ulizwa juu ya tuhuma hizo alikanusha kutenda kosa na kesi yake iliahirishwa hadi itakapo somwa tena march 26 mwaka huu.
Comments
Post a Comment