WALEGWA WA TASAF MPWAPWA WATAKIWA KUBADILIKA.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa Tasaf wilayani Mpwapwa bi Jaribu Mtwange akiwa kwe nyumba yake kabla hajajenga nyumba.
Ofisa ufuatiliaji wa TASAF wilayani Mpwapwa
mkoani Dodoma bwana Hosea Sichone
amewataka wawanufaika wa mpango wa kunufaika na kaya maskini Tassaf wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kutimiza
masharti ya Mpango huo ikiwemo kusomesha watoto na kuboresha huduma za afya ili
kuweza kuwa na mafanikio yaliyo kusudiwa ya mpango huo.
Sichone aliyasema hayo mjini hapa katika zoezi la uhuwilishaji
wa fedha katika malipo ya fedha kwa walegwa kwa kipindi cha mwezi March –Apri 2018.
Aidha
Sichone amesema kumekuwa na upotoshaji
mkubwa kutoka kwa jamii kuwa serikali
inatoa fedha hizo bure tu kwa walegwa kitu alicho kisema kuwa madhumuni ya
mpango huo ni kuziwezesha kaya
maskini sana kuongeza matumizi muhimu
kwa njia endelevu kuziwezesha kaya hizo
kuwa na pesa za matumizi wakati wa hari,
Ameongeza kuwa pia madhumuni mengine ni kuwekeza katika rasilimali watu hasa watoto katika Nyanja ya Elimu na Afya
ikiwa na lengo la kuaandaa kizazi chenye tija ,kuimarisha shughuli za kuongeza kipato na kuongeza
shughuli za huduma za jamii.
Hata hivyo Sichone alidai kuwa
mpango huo tangu uanze kutekelezwa mwaka 2014 umeweza kusaidia wanufaika
wengi kwa kuongeza makazi bora ,kuongeza kipato cha familia lakini imeongeza ari ya akina mama kutojifungulia
katika mikono salama ya manesi na si kwa wakunga wa jadi na majumbani.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa Tassaf
wilaya ya Mpwapwa Paskal Jeremia alisema
kwa Mpwapwa ina walegwa 5993 katika vijiji 57 vya wilaya ya Mpwapwa .
Pia alisema kwa wezi marcha –April wameweza kutoa kiasi cha shilingi milion 370
ambazo ni malipo ya ajira za muda na
malipo ya masharti kwa walegwa.
Mmmoja wanufaikawa Mpango huo kutoka katika
kijiji cha Idilo bi Judith Nohnya alisema kuwa katika maisha yake alikata tama
kuwa asingeweza kujenga nyumba ya bati alkini alisema “ baada ya mpango huu
kuanza kwa kweli nilikuwa na nyumba duni ambayo niliezekea udongo (tembe)
lakini sasa baada ya kuanza kupokea fedha hizi nimenunua mabati 16 na na
nimeezeka nyumba yangu bati na sivujiwi tena”alieleza kwa furaha Bi Judith.
BI
Judith ameiomba serikali kuziondoa changamoto
ndogondogo zinazo ukabili mpango huo kama ucheleweshaji wa malipo ya
ajira za muda na kuwapo na mfumo mzuri
wa malipo kwa watu wote wenye sifa za mpango huo kulipwa fedha zao na
kuwaongeza baadhi ya watu ambao wana shida lakini hawajaingizwa kwenye Mpango.
Comments
Post a Comment