MAENDELEO YA MPWAPWA YAMNYIMA USINGIZI DC,AWATAKA WACHIMBAJI WALIPE KODI.
SERIKALI wilayani Mpwapwa Mkoni Dodoma imewataka wachimbaji
wadogo wa madini Kuweza kulipa kodi
ya serikali ili kuweza kufikia Tanzania
ya Viwanda na uchumi wa kati ifikakapo
2015.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana
Jabir Shekimweri alipokuwa akifunga mafunzo ya siku moja yaliyo andaliwa na shirika
la wachimbaji madini Wanawake Tanzania(TAWOMA)
Shekimweri alisema kuwa kuwa Mpwapwa pamoja na kujaliwa madini ya aina nyingi na yadhamani lakini wilaya
hiyo aiendani na maendeleo
yalikuwanayo kitu alichosema kuwa
kinatokana na matumizi mabaya ya
rasilimali hizo au usimazi mbovu wa rasilimali hizo au matumizi mabaya mali hizo ambayo ni za
watanzania wote.
ALISEMA “ukiangalia Mpwapwa haiendanani na hostoria ya wilaya hiyo kimaendeleo japo kuwa na kuwa
na Neema ya wilaya hiyokujaliwa vitu vingi sasa nataka mlipe kodi ya serikali
ilitufikie uchumi wa viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025,lakini tukilipa
kodo kwa tutaboresha miradi ya maendeleo ikiwemo reli ya mwendo kasi yaani
standand gage”aliongea Shekimweri.
Mmoja wa wachimbaji wa madini Wilayani hapa Bi Elizabeth
Pagama alisema tangu uongozi wa awamu ya Tano iingie madarakani hasa Rais Dkt Pombe
Magufuli amekuwa akiwajali wachimbaji wadogo na kutaka
wachimbaji hao wachimbe kwa
Tija na kufuata sheria za madini
kuwezesha serikali kupata kodi yake kupitia madini yanayo chibwa ndani ya nchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini Wanawake
Tanzania Bi Eunice Negele amesema wachimbaji wadogo wa Madini
endapo wataweza kulipa kodi ya
shughuli wanazo zifanya kutaweza
kutambulika na kuaminiwa na Serikali.
Bi Negele alisema kwa sasa
wachimbaji wadogo wamekuwa na
mtazamo hasi kwa serikali kutokana kuwa ni wakwepaji wa kodi kitu walicho kisema
kuwa mkanganyiko wa sheria za madini kuwa walipe wapi kunapelekea wachimbaji wadogo kuonekana kama sio walipaji kodi.
“Sisi tuaambiwa kama
hatulipi kodi lakini lazima watendaji wa vijiji na kata wajengewe uwezo na
sheria za madini juu ya ulipaji kodi za
vijiji,halmasahauri, na seriakli kuu kitu kinacho tuchanaganya”aliongea Bi Negele.
Bi Negele alisema kwa
sasa japo kuwa nchi ya Tanzania inahesabika kuwa na aina nyingi
za madini na wachimbaji wengi lakini
lakini idara hiyo imechangia kwa asilimia 3% tu pato katika bajeti ya serikali .
Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo mkoani Dodoma (DOREMA) bwana Kulwa Mkalimoto aliomuomba uongozi wa wilaya kuwapo ulazima wa mfumo mzuri wa ukasanyaji wa kodi
na mapato yatokanayo na madini kwa sasa
kitu alicho kisema kuwa kinaishia
mikononi mwa baadhi ya watendaji amabao sio waaaminifu.
Bi
Doreen Kissia mchimbaji wa kopa katika kijiji cha kinusi alisema kero wanazozipata kutoka kwa uongozi wa serikali kwa sasa ni
kutozwa kodi ambazo hazipo kisheria
na hutozwa na watu ambao si wahusika
halali.
Aidha Bi Kissia alisema matatitizo ya namna hii
kwa mkoa wa Dodoma hasa wilayani
mpwapwa yanaonekana kuwa sugu japo kuwa
wizara ya nishati na madini kutoa mafunzo
ya sheria ya madini na kanuni zake ambayo viongozi waandamizi wa wialaya hii walihudhuria mafunzo hayo.
Aliongeza kuwa taratibu zinavyozidi kuvunjwa na baadhi ya
watendaji kwa maslahi yao,
wanaweza kusasababisha uvunjifu wa amani sehemu za migodini hasa kwa wachimbaji
wadogo.
Bi Dorren aliiomba serikali kuweza kuharakisha uuandaji wa tume ya uchunguzi wa kusafirisha madini nje ya
nchi hivyo ili kuweza kuokoa mitaji yao ambayo tangu serikali iweke katazo la
kusafirisha madini nje ya nchi wamekuwa hawafanyi kazi na kusababisha kula mitaji na baadhi yao mitaji yao imekata.
Pia alisema urasimu
huo unaoendelea kwa wachimbaji wadogo utakwamishwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na malengo ya taifa ya Tanzania kufikia kipato cha kati ifikapo
mwaka 2025.
Na aliongeza kuwa japo kuwa
Dodoma kuwa na aina nyingi za
madini yanaweza kuinua hali ya maisha ya wananchi
na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa lakini halmashauri ndio zinazorudisha nyuma
juhudi hizo kutokana na urasimu
uliopo.
Comments
Post a Comment