WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA DODOMA.
Jeshi la polisi mkoani Dodoma
limekamata wahamiaji haramu 64 ambao ni raia wa Ethiopia pamoja na madereva
wawili waliokamatwa katika eneo la Chenene wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakitokea
nchini Kenya kuelekea nchini Afrika kusini .
Watu hao walikamatwa walikuwa kwenye
roli lilosheheni mabox ya maji kwa ajili ya kuwaficha wahamiaji hao ambapo wamekutwa
wakiwa na kiasi cha fedha taslimu zaidi
ya shilingi milioni 5.
kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles
Muroto amesema wahamiaji haramu wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za
udanganyifu ambapo amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahamiaji
haramu wanaoingia nchini.
Peter Kundy ni Naibu Kamishna wa
Uhamiaji mkoa wa Dodoma amesema jeshi la uhamiaji mkoa wa Dodoma limejipanga
katika kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu linaloonekana kushika mkoa wa
Dodoma hapo.
Kutokana na hayo wito unatolewa kwa
wananchi kuendelea kutoa taarifa za uwepo wa wahamiaji haramu nchini ili
kudhibiti kitendo hicho.
Comments
Post a Comment