Posts

Showing posts from 2018

LUFU WAPATA BARABARA TANGU UHURU.

Image
SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma   imewataka wakazi wa kata za Mwanawota na Lufu   waliopatiwa fedha za ukarabati   wa barabara kuthaminisha ukabarabati wa barabara hizo   sambamba na uboereshaji uchumi wa kata zao kwa kufanya kazi kwa Bidii. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa   Jabir Shekimweri alipotembelea   barabara hizo kwa ajili ya kuangalia hali halisi ya ukarabati unaoendelea   katika kata hizo chiniya wakala wa barabara Vijijini TARURA Wilaya ya Mpwapwa. Barabara zilipatiwa fedha za ukarabati   ni barabara ya kibakwe ,Mwanawota yenye urefu wa kilometa 16 yenye dhamani ya shilingi shilingi milion 713,000,000/= na barabara ya kata ya Rufu yenye urefu   wa kilometa   kilometa 16 pia Shekimweri alisema   hakuna zaidi kwa kata hizi kutoa shukrani kwa serikali   ya awamu ya tano zaidi ya kupandisha kiwango cha uchumi katika kata zao   ambazo zimepatiwa fedha za ukarabati. “...

UHARIBIFU WA MAZINGIRA WATISHIA JAGWA.

Image
  Baadhi ya akina mama wakipanda mti katika kata ya Mazae KUFUTIA uharibifu mkubwa wa mazingira   unaofanywa na watu katika   wilaya ya   Mpwapwa   kunatishia   kupungua kwa   upatikanaji wa   huduma ya maji   kwa baadhi ya vijiji vya wilaya ya Mpwapwa. Hali hiyo imetanabaishwa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri kwenye   kilele cha siku ya   mazingira   duniani iliyofanyika katika kijiji cha Idilo kata ya Mazae. Shekimweli amesema   uhai na ustawi wa wa   Taifa letu unategemea   sana   mazingira   yanayotuzungunguka   hivyo alisema uharibifu wa mazingira   ni moja   kati   ya tishio   kubwa la uhai wa binadamu na viumbe vingine   vinavyo tegemea mazibgira   katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Aidha Shekimweri amesema   mabadiliko ya   ya tabia   ya nchi   sasa   yamekuwa ni tishio   la us...

PAROKO KANISA KATOLIKI ATAKA HUDUMA ZA JAMII KUBOREKA MPWAPWA.

Image
Paroko wa kanisa Katoliki Parokia ya Mpwapwa  Pd Daud Ngimba  akihubiri anisani . PAROKO wa kanisa katoliki Parokia ya Bikira Maria wa Fatima Mpwapwa jimbo   kuu la Dodoma Padre Daud Ngimba imeitaka jamii ya   watu wa Mpwapwa na viongozi wa Serikali   kuweza kutumia fursa ya Serikali kuhamia Mkoani Dodoma   kuboresha huduma za kijamii kama ,   Barabara,shule , Afya na huduma za maji   wilayani hapo. Padre Ngimba aliyasema   hayo mwishoni mwa wiki    alipo kuwa akitoa mahubiri   kwenye Misa ya   Utatu mtakatifu   na alipokuwa akiutambulisha mkakati wa kanisa hilo katika kujikita katika utatuzi wa changamoto zinazo ikabili jamii ya Mpwapwa. Padre   Ngimba alisema wakristu ,Tasisi za dini    pamoja na serikali za mitaa katika mkoa wa Dodoma   zitaweza kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuhamisha makao makuu ya serikali kuja Dodoma n...

DARAJA LA GODEGODE LITAFIFISHA MAPATO YA HALMASAHAURI.

WANANACHI wa kata ya Godegode,Pwaga na Lumuma wameiomba serikali kuweza   kurudisha mawasiliano   ya barabara    baada ya   daraja   la Godegode   ambalo ni kuungo muhimu kati ya kata hizo   na makao makuu ya wilaya   kusomwa na maji   katika msimu   wa mvua mwaka huu. Wanachi wa   kata   hiyo   wametoa   ombi hilo mbele ya naibu waziri wa ujenzi   Mhe Eliasi Kuandikwa (MB) alipokuwa kwenye   ziara   ya   kukakuga ujenzi wa barabara za Mpwapwa na kufika katika   daraja hilo   kuangalia   hali harisi ya   changamoto ya   usafiri katika eneo hilo. Diwani wa kata ya godegode Bwana Tanu Makanyago amesema daraja hilo ambalo ndio muhimili   mkuu wa   mawasiliano kati ya   kata ya Godegode,Pwaga, na Lumuma kwa mawasiliano . Aidha Bwana Mkanyago  amesema kutokana na uharibifu   wa daraja hilo   kumepelekea maisha ya watu wanaois...

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI INATISHIA AFYA ZA KINA MAMA.

JAMII imeshauriwa kuziamini   tafiti za kitaalamu   zitolewazo na   Serikali ili kuweza kujiletea maendeleo endelevu au kupunguza athari zinazo weza kujitokeza siku za   mbeleni. Kauli hiyo imetolewa   wilayani Mpwapwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa na Mratibu wa   masuala ya magonjwa ya Saratani   Dkt,Angel Msaki alipokuwa   akiongea   na Majira fisini Kwake   jana. Dkt,Msaki alisema serikali ikiwa katika    mkakati   mkubwa wa    utoaji wa kinga   ya   saratani ya mlango wa kizazi   bado kwa wilaya ya Mpwapwa kunaonekana mwamko kuwa duni na kutishia   watu wengi kuto fikiwa   na   na zoezi hilo. Aidha Dkt. Msaki alidai kuwa    tangu    huduma hizo zianze   kutolewa   hosptalini hapo    kuanzia julai 2017 ni akina mama 530   walifikiwa na huduma   hiyo na kati hayo akina mama   18 walipatikana na   dal...

BABA AMBAKA MWANAE WA MIAKA 12 NA KUMMPA MIMBA.

Mtu mmoja   aliyefahamika kwa jina la Jemsi Leuna mkazi wa kijiji cha Chitemo wilaya   ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma    amefikishwa mbele ya hakimu makazi mfawidhi   bi Nurupedesia Nassar kufutia tuhuma ya kumbaka na kummpa mimba mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa nne. Mwendesha mashitaka wa polisi Bwana Michael Joseph   aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo akitambua kuwa   huyo ni mtoto wake wa kumzaa aliweza kumbaka   na   kutenda kosa hilo kinyume na   kifungu cha namba 130 kifungu kidogo(1) na kifungu 131kifungu kidogo(1)iliyo fanyiwa malejeo mwaka 2002. Bwana Machael   aliiambia mahakama   kuwa kosa la pili   ni kummpa mimba mwanafunzi darasa la nne kinyume na   sheria ya Elimu namba 353 kifunfu cha 60Akifungu kidogo cha kwanza   iliyofanyiwa malejeo mwaka 2016. Mtuhumiwa alipo ulizwa juu ya tuhuma hizo alikanusha kutenda kosa    na kesi yake iliahirishwa...

WALEGWA WA TASAF MPWAPWA WATAKIWA KUBADILIKA.

Image
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa Tasaf wilayani Mpwapwa bi Jaribu  Mtwange  akiwa kwe nyumba yake kabla hajajenga  nyumba. Ofisa ufuatiliaji wa TASAF wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma bwana Hosea Sichone   amewataka wawanufaika wa mpango wa kunufaika na kaya maskini   Tassaf wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kutimiza masharti ya Mpango huo ikiwemo kusomesha watoto na kuboresha huduma za afya ili kuweza kuwa na mafanikio yaliyo kusudiwa ya mpango huo. Sichone aliyasema    hayo mjini hapa katika zoezi la uhuwilishaji wa fedha katika malipo ya fedha kwa walegwa kwa kipindi cha   mwezi March –Apri 2018.   Aidha Sichone amesema   kumekuwa na upotoshaji mkubwa   kutoka kwa jamii kuwa serikali inatoa fedha hizo bure tu kwa walegwa kitu alicho kisema kuwa   madhumuni ya   mpango   huo ni kuziwezesha kaya maskini   sana kuongeza matumizi muhimu kwa njia endelevu   kuziwezesha kaya hizo kuwa na pesa za matumizi wa...