SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI INATISHIA AFYA ZA KINA MAMA.
JAMII imeshauriwa kuziamini
tafiti za kitaalamu zitolewazo
na Serikali ili kuweza kujiletea
maendeleo endelevu au kupunguza athari zinazo weza kujitokeza siku za mbeleni.
Kauli hiyo imetolewa
wilayani Mpwapwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa na Mratibu wa masuala ya magonjwa ya Saratani Dkt,Angel Msaki alipokuwa akiongea
na Majira fisini Kwake jana.
Dkt,Msaki alisema serikali ikiwa katika mkakati
mkubwa wa utoaji wa kinga ya
saratani ya mlango wa kizazi bado
kwa wilaya ya Mpwapwa kunaonekana mwamko kuwa duni na kutishia watu wengi kuto fikiwa na na zoezi
hilo.
Aidha Dkt. Msaki alidai kuwa
tangu huduma hizo zianze kutolewa
hosptalini hapo kuanzia julai
2017 ni akina mama 530 walifikiwa na huduma hiyo na kati hayo akina mama 18 walipatikana na daliiza awali
za mlango wa kizazi na akina mama 10
walifanyiwa matibabu ya ugandishaji na akina mama 25 walipewa rufaa kwenda kuchunguzwa katika
hospitali kubwa kutokana na kudhaniwa
kuwa na saratani hiyo.
“ Kwa Mpwapwa tatizo
ni kubwa kiasi kwamba kwa mafano kati ya
watu 530 waliopiwa ni watu 43
waligunduika kuwa na dalili hizo lakini wengine walidahaniwa kuwa na saratani kabisa ambapo ni sawa na asilimia 8% hadi 9% ya watu wote walio pimwa.”alieleza
Dkt Kihologwe.
Alisema chanzo cha tatizo hilo ni akina mama
kuanza kujihusisha na mahusiano
ya kimapenzi wanali na umri mdogo,au
kuwa na wapenzi wengi ,au kuwa na mume mwenye wapenzi au wake wengi na watu
wanao ishi na virusi vya ukimwi alisema
wako hatarini kupata maambukizo hayo.
Pia alisema tatizo linaonekana ni kubwa kwa wilaya ya Mpwapwa
kutokana na Mpwapwa kukabiliwa na ndoa
za utotoni na hivyo watoto wengi
kujiingiza kwenye mahusiano wangali umri
na viongo vyao havijakomaa kwa ajili
mahusiano ya kimapenzi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Jemsi
Kihologwe alisema kuwa saratani ya
mlango wa kizazi ni mabadiliko ya ya ukuuaji
wa seli za mlango w kizazi ambayo husababishwa misuli au viongo vingine ndani ya utumbo figo na sehemu zingine za mwili.
Dkt Kihologwe alisema
tatfiti zilizofanywa na shirika la afya Duniani ( WHO )lilibaini
kuwa saratani ya mongo wa kizazi lina athari kubwa “ ambapo kila mwaka inakadiliwa akina mama 466,000
wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na wengi wao wako katika nchi zinazo
endelea”alifafanua Dkt Kihologwe.
Pia alaisema kwa Nnchi
ya Tanzania ni saratani inayo ongoza kwa kusasababisha vifo vya akina mama wengi ikifuatiwa na
saratani ya matiti ambapo husababisha
zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote hapa nchini.
Alisema mkakati wa
serikali sasa ni kutoa chanjo kwa
wasisichana wote wenye miaka
14 ili kuweza kuwakinga na saratani hii ya mlango wa kizazi na
wanakusudia kuwafikia wasichana zaidi 51378.
Comments
Post a Comment