WAKAZI WA KIBAKWE WAPATA CHUMBA CHA UPASUAJI.
wakazi wa kibakwe WAKAZI 82,703 wa tarafa ya Kibakwe wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma watanufaika na huduma za upasuaji mala baada ya kukamilika kwa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha tarafa hiyo. Kwa mujibu wa mganga mkuu wa wilya Dkt ,Said Mawji amesema kuwa chumba hicho cha upasuaji ni moja wapo ya miradi ya maendeleo ya afya iliyo anza kutekelezwa katika katika mwaka wa fedha wa 2013/2014. Mawji alisema mala bada ya kukamilika kwa chumba hicho kitasaidia wagojwa wa tarafa hiyo waliokuwa wakipewa rufaa kwenda kufanyiwa upasujai katika hospitali ya wilaya na kupunguza usumbufu kwa wagonjwa na kuokoa maisha ya akina mama na watoto. Aidha Dkt Mawji alisema jengo hilo japo kuwa lilikamilika muda mrefu lakini halikunza kutumika kutokana na ushauri wa kitaalamkutoka ka timu ya uendeshaji wa shughuli z...